Hivi kiswahili sahihi ni osha mikono au nawa mikono? Naona kama tunakosea lugha

Hivi kiswahili sahihi ni osha mikono au nawa mikono? Naona kama tunakosea lugha

Freed Freed

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2017
Posts
6,547
Reaction score
7,167
Tangu ujio wa corona au covid 19, kumekuwa na matumizi ya neno osha mikono.

Mimi navyojua kuosha inahusisha vyombo na viungo nusu vya binadamu tunatumia Nawa. Ikiwa ni mwili mzima tunatumia neno Oga. Kwa nguo tunatumia neno Fua.

Wadau naomba mnitoe matongotongo kwa wale wajuvi wa lugha adhimu ya kiswahili.
 
Sasa hivi ni mda wa kutumia neno lolote maana hali ni tete🤣🤣🤣


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom