Hivi kitambulisho cha mpiga kura naweza kukifanyia nini cha ziada ukiachana na kupiga kura?

Hivi kitambulisho cha mpiga kura naweza kukifanyia nini cha ziada ukiachana na kupiga kura?

Melki Wamatukio

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2022
Posts
6,156
Reaction score
10,974
Habari wanajamvi,
Ukiachia mbali kupigia kura 😆🤤 Hivi kitambulisho cha kupigia kura kinaweza kuwa na matumizi mengine ya ziada?

Au niache kujisumbua kwenda kupanga foleni bure!
 
Ukaombea cheti cha kuzaliwa kama huna.
Ila kwenye huu uandikishaji unaofanyika sasahivi hakuna cheti chochote kinachotolewa wanakuandikisha tu kwenye daftari lako halafu unaondoka hawakupi chochote na wewe hutoi chochote zaidi ya kutaja majina yako 3 miaka na kisha kusaini
 
Huu si ni uchaguzi wa serikali za mitaa! Ina maana hatutajiandikisha kielektroniki kwenye mfumo wa kuwachagua viongozi wa nchi, majimbo na tarafa?
 
Huu si ni uchaguzi wa serikali za mitaa! Ina maana hatutajiandikisha kielektroniki kwenye mfumo wa kuwachagua viongozi wa nchi, majimbo na tarafa?
Mkuu mbona hii nchi haina mfumo wa kuchagua viongozi wa majimbo na tarafa?
Any way kwa kifupi tu kwa sasa kuna zoezi la kujiandikisha kwa ajili ya kuchagua viongozi wa ngazi ya chini wenyeviti wa mitaa na vijiji.
Mimi nimejiandikisha nasikilizia utaratibu sijui siku ya kupiga kura tutaelekezwa nini kwamba tutahitajika.na kuwa na kitambulisho chochote kuonyesha kwamba wewe ndiye mhusika au itakuaje.
Halafu mwaka kesho ndio kutakuwa na uchaguzu wa kuchagua madiwani wa kata, wabunge wa majimbo na Rais utaratibu wa uchaguzi huu bado haujawekwa wazi kwamba watasajili namna gani.
Ni hivyo tu ndugu hakuna kitambulisho wala usajili wa kielectronic kwa sasa mimi nilisajilia sijua kuandikishwa manually nikatoka nje nikakutana na vijana wa uvccm nao wakaomba wanisajili kwenye kidaftari chao cha kawaida wakaniambia mimi natokea shina namba 4 hata silijui hilo shina ila nikawakubali nao wanisajili wakaniahid kutakuwa na mambo mazuri hao madogo wananijua vizuri sana wananijua halafu ni mtata na pia sina chama ni mpinga siasa za kijanja janja.
 
Back
Top Bottom