Hivi kiungo kikuu cha pilau ni kipi hasa..??!

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
38,920
Reaction score
44,970
Natamani kufahamu hivi ni spice ipi hasa inayoifanya pilau iwe pilau...
 
Leo kuna nini ? mwenzio kauliza haki ya kuchinja wewe unauliza viungo vya mchele. Peleka hii Manzese kwa wenzio. mxiuuucvfd
 
Inasemekana eti we ni kiungo cha kutengeneza mchuzi wa mbwa.., eti ni kweli..?!
 
Leo kuna nini ? mwenzio kauliza haki ya kuchinja wewe unauliza viungo vya mchele. Peleka hii Manzese kwa wenzio. mxiuuucvfd
Kwa hiyo wewe unajifanya nini kwa kutapika kinyesi kama hiki..?
 
Sasa umeuliza umepewa jibu unabishana vipi mwenzetu?

Hivo alivokujibu ni kweli kabisa spice kuu ya pilau ni uzile au jina jengine bizari ya pilau wazungu wanaita (cummin)
U mean binzari au..?!
 
Natamani kufahamu hivi ni spice ipi hasa inayoifanya pilau iwe pilau...

Nadhani mkuu pilau ili iwe pilau lazima viungo vyote vikamilike kwa sababu vikichanganywa ndio inapatikana ile ladha na harufu ya pilau...kwa sababu ukiniambie niache vipi kati ya...na kuna tofauti vipo viungo lazima viwe grinded na vingine sio lazima.
Tangawizi (Ginger)
Vitunguu saumu (Galic)
Chumvi(salt)

Binzari nyembamba (CUMIN)
Pilipili manga (Black papper
Iliki (Cardamom)
Mdalasini (Cinamon)
kama utapenda karafuu kidogo

Ni kama uniambie katika meno yako unataka lipi tulipunguze na-ni lazima tufanye hivyo...Nitasema toa la mwisho kwa sababu hapo mbele nikicheka itabidi niweke mkono...lkn itabakia kuwa na meno pungufu hata km nikitoa gego.
 
Pilau ili iwe pilau lazima viungo saba. Viwepo kwa mchanganyiko sawia, yaani kulingana na ukali wa kila kiungo. Binafsi nikipika pilau nahakikisha nina viungo hivi saba ukitoa chumvi, mafuta na kitunguu maji,
Giligilani ya mbegu, mdalasini, pili pili manga, karafuu kidogo, hiliki, binzari nyembamba, na kitunguu saumu
 
jajajajajajaja....huyo wa kwenye avatar ni wewe mwenyewe da mkubwa?
 
Pilau ili iwe pilau lazima viungo saba. Viwepo kwa mchanganyiko sawia, yaani kulingana na ukali wa kila kiungo. Binafsi nikipika pilau nahakikisha nina viungo hivi saba ukitoa chumvi, mafuta na kitunguu maji,
Giligilani ya mbegu, mdalasini, pili pili manga, karafuu kidogo, hiliki, binzari nyembamba, na kitunguu saumu

Me sipendi mbegu za giligilani na pilipili manga kwenye pilau...
Nikipika huwa naweka binzari nyembamba, mdalasini na iriki kidogo....tena navisaga mwenyewe....simple!
 
Unavopendelea wewe tu, nami natwanga mwenyewe mchanganyiko huo baada ya kupitisha kwenye kikaango vikauke vizuri na viblend vizuri wakati wa kutwanga. Tunatofautiana kuonja kwetu, wengine hampendi viungo baadhi wkt wengine vikikosekana au kuzidi tunagundua kitu hakipo sawa sawa na tunavotaka.
 
Back
Top Bottom