Jamani, katiba ni sheria ambayo inatoa mwongozo juu ya sheria nyingine zote ambazo kwa kuzihesabu ni zaidi ya 500. Sasa si lazima kila kitu kielezwe kwenye katiba na zaidi ni katiba hii hii ndio inayotoa mamlaka ya sheria nyinginezo kufanya kazi na watu kuzifuata ilimradi hazipingani nayo, sasa kwa hoja ya mgomo ktk katiba imeelezewa haki ya mtu kujieleza na kuwasilisha maoni(right to freedom of expression) chini ya ibara ya 18, na kama ni mgomo wa wafanyakazi sheria ya Ajira na Mahusiano kazini, Sura ya 366 kama ilivyorudiwa mwaka 2004 imeeleza chini ya kifungu cha 75 kuhusu haki ya mfanyakazi kugoma kufanya kazi au mwajiri kugoma kutoa kazi kwa mfanyakazi wake ili mradi afuate procedures zilizowekwa.