Hivi kumiliki gari ya safari ndefu Kama Toyota Prado kwa safari fupi za mjini ni akili au ujinga?

Toyota Prado ni gari mahususi ambayo imetengenezwa kwa ajili ya safari ndefu Sio mizinguko mifupi fupi ya mjini.Hivi mtu kumiliki Hilo dude kwa safari za mizunguko ya mjini Ni akili au ujinga? Sio matumizi mabaya ya pesa ?


Umaskini wa akili ni mbaya sana...
 
Sijaona sehemu hilo gari limeandikwa la masafa marefu. Na mbona kuna watu wanaenda safari ndefu na passo?

Ulitaka atumie gari gani hapa mjini??

Hela yake kwanini umpangie matumizi??
ni umaskini na wivu wake tu...msamehe
 
Toyota Prado ni gari mahususi ambayo imetengenezwa kwa ajili ya safari ndefu Sio mizinguko mifupi fupi ya mjini.Hivi mtu kumiliki Hilo dude kwa safari za mizunguko ya mjini Ni akili au ujinga? Sio matumizi mabaya ya pesa ?
Mawazo yako...
 
ni ujuha, nina jiran yangu analo huwa analiwasha jumapil tu akiwa anaenda kanisani, weekdays ana ki-makonda chake anabanana na mkewe mwanzo mwisho...mimi nna rush yangu saaafi full burudan
Ngoja niendelee kuwasoma watetezi wa wanyonge, Hii ni Tanzania ya wanyonge.
 
Gari yangu ni 650cc tu ila ninavyowakwamisha humo bara barani sio poa... Wengi na ma Prado yao huwa wanakasirika sana jinsi navyowaovaertake!
Utakua unaendesha possibly Terrios kid/suzuki kei/mitsubishi pajero mini/suzuki carry/suzuki every

Pole sana bro,ni maisha tu na kujifariji ni jambo la maana kwny maisha mkuu.
 
Unakuta mtu ana Nissan navara anaendea kazini
Wacha huyo huyo ana nafuu Kuna wale wanaenda na magari ya mizigo yaani Toyota pickup zile za kubeba majani ya ng'ombe na kupakia mizigo ofisini.Kuna haja iweko dress code ya magari kuwa mtu aende ofisini na gari gani siku ingine mfanyakazi ataenda ofisini na trekta lenye tela au tingatinga ofisini
 
Gari yangu ni 650cc tu ila ninavyowakwamisha humo bara barani sio poa... Wengi na ma Prado yao huwa wanakasirika sana jinsi navyowaovaertake!
Hongera bana kwa kumiliki Terios Kid ama Cami mzee baba. Cha muhimu umekalia chombo cha moto, mwamuzi mkojo wa MwarabuπŸ˜†
 
Uchumi ukiwa mzuri hata kwenda sokoni na scania 113 ni sawa tu.ikiwezekana hata kutumia trector aina ya Ferguson town trip,kuchaguliana usafiri sio vizuri mjini hapa
Hahahah umenikumbusha mbali mkuu, hizo ndio zilikuwa pigo za watoto wa kiarabu watoto wa Mzee Sadiq, Balhabou enzi hizo kishule shule mwana anakuja na horse ya Scania anapark anaingia darasani hana habari.

Mwengine kapewa adhabu alime, anatoroka anaenda kuchukua tractor kwao...kuna watu wana kiburi ya hela mzee. Anaingiza tractor anakichafua mwalimu anabaki anatoa macho tu *****.

Hahah yani ilikuwa vituko tu *****, mwana kaja class kabeba madaftari mawili kwenye shangazi kaja.πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ huku chini ana gum boots jua kalii.
 
ni ujuha, nina jiran yangu analo huwa analiwasha jumapil tu akiwa anaenda kanisani, weekdays ana ki-makonda chake anabanana na mkewe mwanzo mwisho...mimi nna rush yangu saaafi full burudan
Wenye magari ya BASHITE utawajua tu...
 
Magari makubwa yanasaidia sana pindi mvua kubwa inapo nyesha tofauti ist yanaweza kwama
We ndio umeongea point sasa, mtoa mada angetumia hii kama basis ya Argument yake ningemuelewa sana yani.
 
Acha JamiiForums iitwe JamiiForums.
Yaani kila mtu humu anamiliki gari dadeki
JF ina watu laki tano ndugu na wote hao wana emails kwa maana wamesoma na wanamiliki simu nzuri. Humu majority ya wanasiasa wapo humu, majority ya wasanii wapo humu, majority ya wahadhiri/lecturers wamo humu, wafanyakazi wa mabenki, wanaofanya kazi za maofisi ya mashirika,serikali,waalimu n.k wamo humu na hao ndio wamiliki wa magari so usishangae mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…