Hivi! kumiliki ukumbi wa starehe ni kosa? Hakuna kiongozi wa CCM anayemiliki biashara ya burudani?

Hivi! kumiliki ukumbi wa starehe ni kosa? Hakuna kiongozi wa CCM anayemiliki biashara ya burudani?

mcfm40

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2010
Posts
4,452
Reaction score
3,151
Ndugu zangu WanaJF,
Kwa siku za karibuni viongozi wengi wa CCM kuanzia wa Wilaya na mikoa mpaka Taifa wamekuwa wakitumia umiliki wa Freeman Mbowe ukumbi wa Bilicanas kama kete ya kuchafuana kisiasa. Alianza Wasira na wengine wote wakafuatia sasa imekuwa km sala ya Baba Yetu. Kina mwanaCCM ameshikilia hapo. Wakikabwa koo wanakimbilia haraka kusema Mbowe ni mpiga Disco.

Nimekuwa najiuliza hivi huko CCM hakuna viongozi wanaojihusisha au kuendesh biashara za burudani? kwa haraka tu bila kufikiria wapo wengi. Nani asiyemfahamu Komba (MB)? Yupo hapo alipo kwasababu ya Bendi ya muziki wa dansi na uimbaji. hizi ni biashara zilizomtoa. Kundi la TOT ambalo kimsingi ni mali ya CCM. Je CCM kumiliki bendi za muziki kama TOT ni aibu au kosa? Wakati ule Mudhihir mbunge wa mda mrefu CCM na kiongozi wa chama alikuwa anamiliki Mchinga Sound (sijui siku hizi anaendesha bendi gani), je ni kosa au hakupaswa kuwa kiongozi? Juma Kapuya aliyewahai kuwa mbunge na waziri kwa muda mrefu alikuwa au anamiliki au ana hisa katika bendi ya nadahani FM academia au Akudo. Je ni makosa au nia aibu kufanya hivo? Mlolongo ni mrefu. Hapa hatujaweka wale wanaomiliki nyumba za kupangisha wageni (lodges) na baa ambazo karibu viongozi wengi wa CCM wanafanya biashara hii. Actually wengi wao hawatumia majina yao halisi. Na wamekubuhu kwa kukwepa kodi. Wanafanya hizi biashara kwa siri.


Hata hivo swali la kujiuliza ni je, kuendesha biashara ya burudani kunapunguza uwezo wa mtu kuwa kiongozi? Kuna mahali kwnye sifa za kiongozi panasema asiendeshe biashara ya burudani? Mbona wanashindwa kuja na hoja walau inayoonesha kwamba Mbowe amekuwa anakwepa kodi au anafanya baishara za udanganyifu ili walau tuseme wana hoja? Wakati mwingine huwa naona kama CCM kumtangaza Mbowe kwamba anaendesha Biashara za Disco sijui nini nafikiri kumfanya aonekana safi mbele ya jamii kwamba kumbe huyu mtu hana makubwa na biashara zake zipo wazi. Hakujificha kwa kutumia ndugu km CCM wafanyavyo ili kukwepa kujulikana.

Wananchi tunachotaka ni uadilifu na uchungu kwa walalahoi, sio biashara gani mtu anafanya. Hata km unauza nyanya ialimradi ni biashara halali haikunyimi uwezo wa kuongoza watu. CCM tafuteni hoja nyingine hii ya mbowe na disco inamjenga zaidi na kumfanya azidi kupendwa kwa sababu anaonekana kufanana na watu wa kawaida zaidi. Nyie endeleeni kutuibia na makampuni yenu ya mafuta na biashara kubwa kubwa na waarabu lakini ipo mtawapigia magoti hawa wapiga disco!!
 
Kama ingekuwa ni kosa, how about TOT, John Komba, Ukumbi wa Vijana Kinondoni na kumbi kibao CCM wanazomiliki?
 
Mwapachu anamiliki The grand chika zamani ilijulikana kama Lacasa chika in Tanga
 
mwingine Mkapa anamiliki Hotel na Kumbi ya Mikutano na starehe inaitwa Irente View iko Lushoto Tanga
 
Dar Live inamilikiwa na nani?

Miaka ya nyuma kulikuwa na bendi moja inaitwa Akudo impact - ilikuwa inamilikiwa na nani?
 
Tatizo mbowe ni dj hiyo ndo tofauti na wamiliki wengine mbn maisha ni ya mh nanihii
 
.. Club ni biashara kubwa sana kiasi kwamba viongozi wengi wa CCM wanaweza kumiliki ndotoni au kwa kutumia pesa wanazotuibia kupitia mikataba mbali mbali tu. Mbowe anatakiwa asifiwe kwa kuiweka Billicanas kwenye chati miaka yote hii maana kuna akina 84 club dodoma wamefulia kiasi kwamba kingilio kimefikia buku 2!
 
Mm nadhan watu wenye fikra fupi ndo wanye kuanzisha mijadala isiyokuwa na tija kwa mwananchi wa kawaida na taifa kwa ujumla badala ya kutuambia mikakati gani watatumia kulikwamua taifa hapa lilipo wanaanza personal attacks halafu zisizo na miguu wala kichwa watu wanataka vifaa mahospitalini,madawa hakuna halafu waziri anaenda kuongelea jukwaani mambo ya kumbi za disco sukari imefika Tshs 2,000/-kwa kilo moja wakati kuna kiwanda hapo Bukoba achilia mbali Mtibwa na Kilombero hawaongei vitu vya msingi na vinavyogusa maisha ya mwananchi wa kawaida ***** tu wanamwaga.
 
Dar Live inamilikiwa na nani?

Miaka ya nyuma kulikuwa na bendi moja inaitwa Akudo impact - ilikuwa inamilikiwa na nani?

Kama kumbukumbu zangu ziko sahihi, Akudo ilikluwa inamilikiwa na Prof.Juma Athuman Kapuya,kirefu chake inadaiwa ni jina lake 'Athman' na majina ya wanae 'Kulwa na Dotto thus, AKUDO.....kuna mtu aliwahi kuniambia hivyo
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Kama kumbukumbu zangu ziko sahihi, Akudo ilikluwa inamilikiwa na Prof.Juma Athuman Kapuya,kirefu chake inadaiwa ni jina lake 'Athman' na majina ya wanae 'Kulwa na Dotto thus, AKUDO.....kuna mtu aliwahi kuniambia hivyo



Upo sahihi mkuu,Pia Professor anamiliki ukumbi wa starehe wilayani Kaliua. Ni ukumbi huu huu ambao mwanaye alimtwanga mtu risasi akafa na kesi yake ikaishiwa kupigwa kalenda na mwisho sijui iliishaje.
 
Back
Top Bottom