Hivi kuna anaye waelewa viongozi wa Simba?

ITR

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2022
Posts
6,096
Reaction score
16,390
Tangu mwanzo mwa msimu timu imekuwa na mwenendo wa kusuasua na kuonesha mapungufu mengi.

Nilitegemea kwenye dirisha dogo la usajili viongozi wa simba wafanye usajili wa wachezaji wenye uwezo kuyafidia mapungufu hayo na kuacha wachezaji mizigo ndani ya timu, lakini cha kushangaza mpaka sasa hakuna cha maana kinacho endelea na dirisha linakaribia kufungwa.

Hapo Congo na Uganda kuna wachezaji wengi wazuri wadogo na wa bei ndogo lakini viongozi wa Simba wamekomaa na wachezaji wa Africa Magharibi tena wazee ili wapate mianya ya kupiga hela.

Yaani pale Simba tangu aondoke Babra na kufariki kwa Hanspope simba limekuwa litimu la hovyo kwenye ngazi za uongozi, na kuna ombwe kubwa la kiuongozi.

Kwa hali hii simba itafukuza makocha wote iwamalize dunia hii.
 
Wewe tulia umeletewa babakar sarr kiungo aliyemkaba Ronaldo unafikiri mchezo si umemuona kwenye michuano ya mapinduzi cup🤣🤣🤣🤣
 
[emoji23][emoji23].... subiri dirisha lifungwe...watangaze
 
Makolo FC Wanaelewa Viongozi Wao Wenyewe.[emoji23]


Ya Caesar Muachie Caesar.
 
Viongozi wa Simba wana mambo ya kiwaki sana
 
Vipi man u itafukuza wangapi?
 
Pale simba pamejaa rushwa ina bidi baadhi ya viongozi pale watiwe ndani kwanza kama akina Aveva na Kaburu, tofauti na hapo simba inaenaelekea pabaya sana.
Uzuri wa mashabiki wa Simba ni wazuri sana kwenye kuipuuza timu inapokuwa na mfululizo wa matokeo mabaya.
 
Dirisha dogo ni vigumu sana kupata wachezaji wazuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…