Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,048
- 22,790
Hivi kuna data zozote kuhusu ugongwa wa Zika Tanzania? Ninakumbuka kuwa sababu kubwa iliopolekea hayati dr Mwele kuachishwa kazi Mhimbili ni kutangaza kuwa Tanzania ina wagongwa wenye virusi vya Zika. Baada ya hapo hatukuwahi kusikia lolote tena kuhusu ugonjwa huo. Sasa kwa vile pande zote mbili zilizovutana katika sakata hilo zimeshatangulia mbele ya haki, ninaomba wataalamu wa afya walioko kwenye jukwaa hili watutangazie kwa kutupatia ukweli halisi.