Hivi kuna maandamano yoyote yaliyoitishwa Tanzania juu ya Serikali kisha yakafanikiwa?

Uko sahihi sana mkuu
 
Jikite kwenye mada
 
Mbona ni juzi juzi tu tumetoka kushuhudia Maandamano ya BAWACHA au mna amnesia?
BAWACHA maandamano gani? Hata UVCCM pia huwaga wanaandamana. Mi sihesabii yale kama maandamano kwa sababu kwanza hayakuwa na ajenda fulani. Mi nachkulia ile kama “Road Walk” tu waliamua kunyoosha miguu. Sidhani kama una umri mdogo wa kutokufahamu maandamano ya kushinikiza Serikali kufanya jambo au kulaani kilichofanywa na Serikali.
 
Ajenda ilikuwa ni KATIBA MPYA.
Narudia tena, sijaona maandamano pale. Ile ni road walk ambayo malengo ilikuwa ni kuelekea mahali ambayo walikuwa wanaenda kukutana kwa ajili ya mkutano. Maandamano hayana hotuba wala speech, ni kukutana mahali fulani, tunaelekea mahali fulani kupitia barabara fulani. Unaandamana kuhusu katiba mpya wakati unaandamana kuelekea ukumbi wa kufanyika mkutano ambako Hakuna hata katibu anaehusiana na masuala ya katiba? Wangeandamana kuelekea hadi Wizara ya katiba na sheria ningejua ni maandamano kweli.
 
Nawe katibiwe kilichomo humo kwenye fuvu lako kama yake matembezi uliyatafsiri kama maandamano
Nini maana ya Maandamano?

Ngoja nikusaidie
Maandamano (kutoka kitenzi "andaa" kilichonyambuliwa kwa viambishi -ma- na -na-; kwa Kiingereza procession, kutoka Kilatini processio, pia cortege) ni kundi la watu wanaotembea pamoja kwa utaratibu maalumu.
 
Sahivi utayaona watu wamechoshwa na huu utawala dhalimu
 
Watanzania hawakufunzwa uhjinga wa vurugu zisizo na msingi.

Imagine ukaandamane Kwa sababu Lisu amekaidi amri ya Polisi,wewe unaweza?
Sio watanzania hawakufunzwa, maana hakuna aliyefunzwa kuwa kondoo, bali kizazi hiki cha watanzania kilipandikizwa uoga, na huo uoga umeendelea hadi sasa. Lakini taratibu kizazi hiki kinaanza kuonyeshwa kuwa uoga wao dhidi ya kigenge kidogo cha wala cake ya taifa ndio hasara yao.

Tutafika huko lazima, maana tawala zinazokaa madarakani kwa shuruti, hutolewa kwa machafuko ama mapinduzi ya kijeshi tu.
 
Arusha kulifanyika maandamano kugomea meya wa mchongo hadi watu watatu wakafariki, matokeo ya maandamano yale ulipofanyika uchaguzi mwingine haikuwezekana kuchakachua tena, na Arusha wakapata meya wa upinzani.
 
Waraka
 
Nini maana ya Maandamano?

Ngoja nikusaidie
Maandamano (kutoka kitenzi "andaa" kilichonyambuliwa kwa viambishi -ma- na -na-; kwa Kiingereza procession, kutoka Kilatini processio, pia cortege) ni kundi la watu wanaotembea pamoja kwa utaratibu maalumu.
Na mimi nilijua tunazungumzia “Protest” na sio “procession” 🤷🏽‍♂️
 
Tofauti yake ni nini?
“PROTEST” ni uelezeaji au tamko la pingamizi la kutoidhinishwa au kutokubaliana ama kupinga jambo ambalo mtu hana uwezo wa kuzuia au kuepuka.

“PROCESSION” ni kikundi cha watu au vyombo vya moto kutembea barabarani au njiani na kwa utaratibu maalum, na mara nyingi huwa kama sehemu ya kuidhimisha sherehe.

Nipe tofauti yako unayoifahamu wewe, mtaalamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…