Hivi kuna maandamano yoyote yaliyoitishwa Tanzania juu ya Serikali kisha yakafanikiwa?

Maandamano ni yenye ajenda Matembezi hayahitaji ajenda.

Yale ya BAVICHA yalikuwa ni Maandamano yenye ajenda ya Kudai KATIBA MPYA.
Nilijitutumua kukupa definitions zote za Procession na Protest kwa kutegemea na wewe ungekuja na definitions ambazo zingejitosheleza kuelezea hicho ulichokiita maandamano kwa jina la procession na sio protest.

Ndio mana mwanzo nilikwambia unahitaji matibabu ya hicho kilichomo kwenye fuvu lako.
 
1. Bado hapajatokea ishu yoyote serious iliyowahi kuwagusa na kuwaumiza Wananchi moja kwa moja.

2. Watanzania wengi hawana uadilifu, so ukitokea ishu yoyote ya kuvunja uadilifu au ukandamizaji hawashtuki sana, kasababu na yeye ameshawahi vunja maadili, ashawah iba, ameshawahi kuomba rushwa iwe ya pesa au ngono, so haumii kihivyo maana nayeye anafanya kt eneo lake.

3. Ukosefu wa Elimu ya kujitambua, hapa watanzania wengi hawajui Km serikali ni mali yao, wanadhan Serikali ni kitu hatari sana na inaweza kujiamria itakavyo.

4. Uoga na ile asili yetu ya kijamaa, inapelekea kuona kila mtu ni ndugu yako, sasa kumpiga au kumpinga kwa nguvu sana itaonesha km unamuonea ndugu yako hivi.
 
Huu sasa ni ubishi hebu rudi tulipoanzia.
 
Wanazitafutaje hizo fedha? Kutoka kwa nani??
 
Tatizo ni HOFU ya watawala.

Wamejipanga kuua yeyote atakayeandamana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…