Sidhani kama kuna mzazi anayependa mtoto ama watoto wake wapitie katika njia isiyofaa ambayo yeye mzazi aliipitia.
Kama wapo wazazi wa aina hiyo, basi hapo kuna mjadala mkubwa sana.
Yote kwa yote, kila mzazi hujaribu kuficha madhaifu yake kadha wa kadha kwa mtoto ama watoto wake ili kuwajenga katika makuzi bora.
Hivyo ni mbinu tu mojawapo ya kimakuzi.