Kutaka kujua mwenye akili timamu na asiye nazo, ni vigumu sana. Ingependeza kwanza mtu akajiuliza mwenyewe jee ana akili timamu, kabla hajatupa swali au kuwauliza waru wa SCAN akili zao.
Unapomsomesha mwanao unataka apate elimu ile awe mtu wa busara na aweza kujijenga kimaisha, au una malengo apate Ajira tuu na hiyo ajira lazima iwe pahali fulani.
Mimi napenda wanangu wawe na elimu nzuri, wawe binadamu wakuishi na wenzao vizuri, wawe wabunifu wenye jitihada na waaminifu, wawe watu wenye utu na msaada kwa Jamie.