Hivi kuna raia wanajivunia kuwa Watanzania?

Tanzania, fahari ya Africa. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika
 
Reactions: Tui
Mpaka TAKATAKA itoke madarakani ndio nitajivunia...sina uzalendo kabisa.

Msema kweli ni mpenzi wa Mungu.
 
Ni maisha tu yanakuvuruga dogo yakikaa sawa utaifurahia hii nchi tamu sana.
 
Reactions: Tui
Laana unayo wewe siyo nchi.
 
Ukiukana tu uraia haliyakua umezaliwa bongo aise utateseka sana, watakufanyia kila hila uione hii nchi chungu
 
Unaichukia nchi mama Tanzania au unachukia wanao-ongoza nchi ?

Tanzania ni nchi nzuri Sana Ila changamoto ipo Kwa waongazaji nadhani hoja yako irekebishwe ili ilete mtiririko mzuri wa mawazo.
 
Wanufaika na ujambazi dhidi ya mali za umma ndo pekee wanajivunia Utanzania wao maana unalipa kwa njia wamazotumia...
 
Kwa hiyo mmeamua kwenda kufungua uzi mwingine kurevenge ahaaa haaa @ diaspora bana, sasa usipojivunia kuwa Mtanzania utakuwa nani? Asili yako ni kitu huwezi kubadilisha.
 
Nawashangaa wanaokataa utanzania wao.Unakuta mtu analalamika tafuta uraia mwingine kama utanzania haukufai.
Hata akipata uraia mwingine haitabadilisha historia yake kwamba asili yake ni Tanzania.
 
Hata akipata uraia mwingine haitabadilisha historia yake kwamba asili yake ni Tanzania.
Saa nyingine mtu inabidi utumie lugha anayoelewa mleta (matamshi) lugha.

Lugha hiyo hiyo anayotumia. sasa akayale matapishi yake na Laana yake.

TANZANIA imebarikiwa. Period. Kama yeye amelaaniwa , alaaniwe mara saba saba na Ukoo wake. Atuachie sie wengine tuliebarikiwa.
 
Reactions: Tui
Ukitaka kujua kama unatakiwa kujivunia kuwa mtanzania ni pale ukipewa nafasi ya kuamua kuukana utanzania na kuchagua nchi moja wapo ya Africa ya kuhamia.
 
Mimi sio mnufaika wa keki ya taifa. Lakini najivunia utanzania.

Utanzania sio mbaya wabaya ni watanzania, majority niwabinafsi, wanafiki, machawa na wenye mihemko.

Ila kwa upande mwingine tuna mazuri yetu. Watanzania wengi hawana roho mbaya kiivyo, ni wakarimu na wacheshi, sio watu wa visasi, na mengine mengi tu.

Siku utaishi ugenini ndo utaijua thamani ya nyumbani.
 
Kitu ni kibaya ukiwa nacho. Siku ukiwa hunacho ndio utajua uzuri wake.
 
Kwa hiyo mmeamua kwenda kufungua uzi mwingine kurevenge ahaaa haaa @ diaspora bana, sasa usipojivunia kuwa Mtanzania utakuwa nani? Asili yako ni kitu huwezi kubadilisha.

Jamaa kachoka raha za bongo anataka kwenda kupata tabu ughaibuni, nampa ushauri wako asiache raha za bongo kwenda kupata tabu huko.
 

Hujatembea nchi za wengine mkuu
 
Labda bongozozo maana ndo mtu pekee anakula dili za serikali kwa sababu ya uzalendo wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…