Tatizo ni katiba iliyopo mkuu. Maana inaelezea idadi ya kura zilizopigwa, haielezei idadi ya walioandikisha kupiga kura.
Hivyo naungana na GeniusBrain kuwa inatakiwa ibadilishwe katiba ya Tanzania, na iwe na amri ya kila aliyetimiza umri wa kupiga kura kujiandikisha kwa lazima, na kupiga kura kwa lazima, kama wenzetu Rwanda walivyofanya. Kama mtu hakupiga kura kwa sababu zisizo za msingi anachukuliwa hatua kali za kisheria. Nasema hivyo kwa sababu kuna jamii ya watu ambao hawataki kushiriki kupiga kura, wao wanataka tu kuchaguliwa viongozi na wengine, jambo ambalo sio nzuri kidemokrasia.