Hivi kuna uhusiano wa kwenda Ulaya na kufeli maisha?


Ewaaa sasa wewe umekutana na wanyamwezi wa kweli afu usikute unaniongelea mimi mkuu 😉
 
Ewaaa sasa wewe umekutana na wanyamwezi wa kweli afu usikute unaniongelea mimi mkuu 😉
Ahaaaaa sidhan maana mmoja nilikutana nae humu na najua id yake, mwingine nilijuana ne mitaani sijui kama yupo humu

Nb naona uko team job tukiandamana kupinga kujiuzulu nitakuunga mkono😂😂😂😂
 
Ahaaaaa sidhan maana mmoja nilikutana nae humu na najua id yake, mwingine nilijuana ne mitaani sijui kama yupo humu

Nb naona uko team job tukiandamana kupinga kujiuzulu nitakuunga mkono😂😂😂😂

😀 😀 tumpe Mwijaku uspika sasa au unasemaje?
 
Ni sawa unapofeli maisha ukaamua kwenda Riaha mbuyuni kulima vitunguu au ukaenda chunya kuchimba dhahabu.

Maisha popote kijana na unapotafuta usione aibu
 
Mimi siko interested na thread bali niko interested na mtuhumiwa namba moja.

Nakupa masaa 24. Vinginevyo utaletwa na pingu

Cc Chaliifrancisco kwa taarifa na utekelezaji
 
Kwani nikifika Dubai kunaniongezea nini?nitolee unga wako hapa
Siku bhana nikapata kasafari ka kikazi Hong Kong. Kuna jamaa zangu wako pale nikasema niwatafute kiaina. Wale jamaa wakajua niko kule lakini akili ikawatuma nimezamia kwenda kutafuta mchongo.... Jamaa walinikwepa sijawahi kuona. Kuja kushangaa wakajua hoteli niliyofikia .... wakashangaa na kuanza kunitafuta....

Wakanipata na wakapatikana kweli.
 
Ulaya ni hapahapa tu.... as long as unajua kuzitafuta....

Sent from my SM-A505FN using JamiiForums mobile app
Mkuu, tudondoshee mbinu angalau chache tu.

Mimi nimejaribu kuuza vipapatio vya kuku na vimbawa lakini sasa vinadoda?

Niliporudi bongo miaka kadhaa nyuma nikaanza na hizo vimbawa niliviita "wicked wings" na tuchips twembamba.

Niliweka kakibanda pale "Kwa Mtogole" lakini uswahilini saa hii hakuna pesa.

Ila hali ya uchumi kwa sasa ni mgogoro.
 
Ni nadra sana kutoboa ukiwa huko, huku mwalimu wa shule ya msingi anamshinda aliyeko huko nje. Mie Kuna ninaowajua wako nje ila wazazi huku nyumbani wanawasaidia.

Mmhh! Mkuu mbona kama una data za side -ve tuu!? Well ngoja nisome comment then nitaandika ninayoyajua kwa side zote mbili.

Ila in short kwenda Ulaya sio kufeli na wala kwenda Ulaya sio kufaulu kama ilivyo kubaki hapa sio kufaulu na wala kubaki hapa sio kufeli
 
Well, nimesoma comments kadhaa ngoja na mimi nichangie, from my experience ulaya kuna makundi matatu ya watafutaji.
1.Wanafunzi.
2.Waliozamia na hawana ujuzi.
3.Waliozamia wana ujuzi.
4.Walioend kwa ajira za makampuni ya kimataifa.

Makundi hayo manne juu usitegemee kama watarudi hapa na maisha sawa kama unavyotegemea kuwa wawe wametoboa.

Kubwa baya zaidi ni kushindwa kuishi kwa malengo.....

Yaani huyo jamaa ako namba 1 inaonekana hana malengo hata pale alipofeli, au ungemuuliza alikuwa na malengo gani ambayo yalifeli hapo ungepata picha y yeye alikuwa mtu wa aina gani huko Yurop.
 
Kwa comments hizi tutaendele kushuhudia watu kama kina Obama wanatokea kwa Wenzetu.
West Africa, mtoto anachangiwa pesa ili azamie, akatafute maish sisi tunasema bora kwetu wakati Africa tunaijua na kwetu tunajua n tunaona palivyo.
Kwa ufupi fighting spirit ya Wabongo wengi nje ni ndogo, mmatumbi anataka kuiishi Paris kama mzungu lazima life likupige K.O
 
Aiseee Bora kudanga Tanzania kuliko kupoteza muda huko Ulaya....rudini tu kwa kweli

Huwezi danga ulaya “labda” nchi za bara la Asia au Uarabuni. Ni sahihi wapo waliofeli na pia wapo waliofanikiwa, wengi wanaorudi huwezi juwa kwa nini wamerudi labda deportion au kaharibu sasa unategemea mtu kama huyo atarudi na nini? Mwingine alikuwa anaishi bila makaratasi so hata kazi unazopata ni za kipato cha chini unaishi kama digidigi. Ungekuwa umeshawahi kufika huko ulaya ungeandika kilicho bora zaidi na ungejuwa kwa nini inakuwa hivyo pia kumbuka wengi wao hawezi kukuambia ukweli kwa nini karudi. Tatizo mlishaaminishwa mtu akienda nje lazima atafanikiwa kumbe hata ndani unafanikiwa tu so mkikutana na aliyetoka nje mnamatarijo makubwa sana kwamba anapesa na amefanikiwa.Kusafiri Nje na kufanya kazi kunakupa exposure na sio guarantee utafanikiwa.Maisha popote!!!!!
 
Haya.maneno mazuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…