Hivi kuna uhusiano wa kwenda Ulaya na kufeli maisha?


Ila marekani hali ni tofauti. Watu hawapendi kupanga maana mifumo ya kumiliki nyumba ni rahisi.
 
Wapangaji ni wengi hata US kuliko wenye nyumba zao. Hii ni kweli kwa kila nchi. Ila ninachosema ni kuwa ile hamu ya kuwa house ower siyo deep km ilivyo kwa Watanzania. Nchi zilizoendelea watu walio wengi hawana nyumba kwa kuchagua, siyo kwa kukosa means.
Ila marekani hali ni tofauti. Watu hawapendi kupanga maana mifumo ya kumiliki nyumba ni rahisi.
 
Mifumo ya huko Ulaya kutojenga Ni sawa,msitufanye hatujui kwamba Ulaya kujenga sio issue,Sasa kufananisha Mambo ya Ulaya na bongo huko Sasa Ni kujizima data.eti kisa Ulaya hawapimi maendeleo kwa kujenga nyumba unaleta kipimo hicho huku bongo,my friends pangeni Sana nyumba mkiwa huko Ulaya Ila jengeni nyumbani mkirudi huku mnakuwa wasumbufu Sana tafadhali mjenge pa kufikia unless mmeamua hamtorudi Tena kuishi huku...mkiambiwa mnakimbilia kutuambia hatuna exposure wakati Kuna wenzenu wako huku wanahangaika kujibanza kwenye nyumba za watu na waliokuwa wana majibu Kama haya yako... wake up
 
Nyie jengeni ili siku mkifa, mnawaachia watoto nyumba. Sisi tutawaachia $$. Cash is king. Wakitaka kununua nyumba, watanunua wenyewe. Kila munu ave na kwao... Mtu amenunua maviwanja kama hatokufa siku moja. Akipata milioni 2, huyo anakwenda Mabwepande kununua kakiwanja... Hana hela benki, amejaza maviwanja tu mikoa mbalimbali! Halafu anajiona mjanja!
 
Endelea kujizima data...kupanga Ni kuchagua
 
Wakachukue elimu warudi, that is the word!
 
nionyeshe kitufe cha kugonga likes mara mbili.
 
Umenena Vyema Sana mkuu....nimependa hapo kwenye"Wake Up Call"nadhani watakuelewa
Yaan wabongo sio hustler kama walivyo wanigeria kwa hiyo ni kama tatizo la kirithi la nchi sisi tumeridhika sana na maisha ndo changamoto kubwa tuliyonayo

Nchi kama marekani, Canada au any western Europe kutoboa ni ngumu kinyama inabid uwe exception a.k.a utumid kipaji ndo utatoboa kirahis, kule competition ni kubwa sana mim mda si walaumu

Wengi wakirudi wanakua na kama Wana mental unstable walichotegemea kule ni tofauti alafu huku tunatarajia makubwa kutoka kwao hio ndo changamoto

Wengi wanaoenda huko ulaya ni watoto wa-kishua wanajua nyumbani Kuna ela, tofauti na wanaoenda south Africa ni watoto wa mbwa kule wanaenda kutafuta Ela ndo maana ni rahisi kwao kutoboa
 
Hizo kazi za amazon usifikirie utani unaweza kufa mapema.. halafu ulaya kodi utawaambia nini.. wengi wanaokuja huku kwa kujilipua wanatumia pesa ya serikali tuu ya ulaya wanazaa watoto hata 7 ili pesa za watoto watumie wao[emoji1787][emoji1787][emoji1787]ulaya kama huna elimu umejiingiza kwenye matatizo makubwa sana huwezi toboa
 
Western world ili uishi vizuri inatakiwa kipaji chako mixa uwe mwanamichezo yaan uwe na kitu Cha utofauti tofauti apo hata kama una degree kumi na sio exception utaishia mediocre na maisha ya stress na depression umo umo kule pagumu sana sio sehemu ya kukimbilia bila kuwa na target
 
Kwasababu tuchukue mtu analipwa mshahara wa 2000€ kazi ngumu, hapo kodi kama huja familia wanachukua chao kama 30% wewe kodi ya nyumba kama mji mkubwa si chini ya 700€ unabaki na nini hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…