Kabla ya kujibu swali, inabidi utuambie kuoa ni nini?
Maana mtu anaweza kujibu swali akiwa na fikra tofauti kabisa ya kuoa na unavyofikiri wewe, mkawa mnakubaliana au kupingana huku hata hamjakubaliana kwamba mnaongelea kitu kimoja au vitu tofauti.
Mathalani, je, unahesabu mwanamme na mwanamke kukaa pamoja bila kushirikisha mipango ya kidini , kimila au kiserikali kwamba ni kuoa? Wengine wanasema huku ni kuoa (common law marriage) wengine wanasema si kuoa.
Na kama unakubali huku ni kuoa, mtu akae na mwenzake kwa muda gani ili wahesabike wako katika ndoa? Nini tofauti ya girlfriend, mchumba na mke wa "common law marriage"
Kuna maswali mengi kama hayo inabidi kujibu kwanza.
Mie naweza kusema kuoa si lazima, kumbe naongelea kuoa kiserikali na kidini, na siongelei common law marriage.
Umenipata hapo?