Hivi, kuna umuhimu wa kikosi Cha Simba kwenda kuweka Kambi Uturuki kujiandaa na msimu mpya?

Noti bandia

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2020
Posts
2,684
Reaction score
4,315
Tumeona misimu miwili Nguvu kubwa imetumika kwenda kuweka Kambi Uturuki kujiandaa na msimu mpya lakini wenzetu Yanga wakijichimbia hapo Kigamboni na maisha yanaenda vizuri tu.

Ni muda sasa muda mwingi na fedha za Kambi ziwekezwe kwenye usajili Bora.
 
Mawazo ya kimaskini utayajua tu!! Ni sawa na maneno ya mke wa maskini anayemwonea wivu jirani yake kwa kupelekwa na mumewe outing Dubai mapumzikoni na kudai kuna umuhimu gani wa kwenda kupumzikia Dubai, ni afadhali mume wangu huwa ananitoa kigamboni kwenda kuona daraja na kurudi zetu Tandale!!
 
Kwa hiyo uturuki mnaenda outing na si kuiandaa timu ifanye vizuri msimu husika?
 
Mawazo ya kimaskini utayajua tu!! Ni sawa na maneno ya mke wa maskini anayemwonea wivu jirani yake kwa kupelekwa na mumewe outing Dubai mapumzikoni na kudai kuna umuhimu gani wa kwenda kupumzikia Dubai, ni afadhali mume wangu huwa ananitoa kigamboni kwenda kuona daraja na kurudi zetu Tandale!!
Akili yako ndogo Sana. Outing ni jambo lisilohitaji return zaidi ya kuifurahia maisha lakini Kwa upande wa football unaenda kuweka Kambi ili kujiandaa na ushindi wa ligi na makombe mengine. Sasa Simba Huwa wanaenda huko Kwa malengo Gani?
 
Wachezaji wazee hata waende wapi kinachotakiwa ni kufanya usajiri unaoendana na wakati huu toeni Wastaafu hao washachoka tafuteni damu changa wakiwashe hapo ninyi sio wa kupigwa gwala ni kwa sababu ya Utura wenu...
 
Kwa hili la kuweka kambi nje Simba na hasa Mo ajitathmini kwani anatupa pesa zake bure. Badala yake hiyo pesa angeongezea kwenye usajili wakati ule akawapata Manzoki, Adebayor, Mo Syilla na Aziz Ki halafu angetafuta kocha wa maana ingewasaidia sana Simba kutimiza ile ndoto yao ya kubeba ubingwa wa Afrika. Kwa sasa kwa timu iliyopo hata kubeba Mapinduzi Cup ni mashaka matupu.
 
Back
Top Bottom