Hivi kuna undugu gani uliopo kati LadyJaydee, Stephen Wasira, Wakazimusic na Ester Wasira

Decree Holder

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2015
Posts
2,559
Reaction score
3,745
Nimekuwa nikiona hawa watu wanne wakiwa karibu sana na kushirikiana sana katika mambo mbalimbali hali iliyonifanya nijiulize kuna uhusiano gani. Najua lazima watakuwa ndugu lakini sijajua ni undugu gani uliopo baina ya Ladyjaydee na Wasira, Wakazi na Ester Wasira. Kiufupi nimependa jinsi wanavyoshirikiana.

UPDATES

Baada ya kuutafuta ukweli nimegundua yafuatayo.

Je wajua kuwa Judith Wambura Mbibo aka Lady Jaydee na rapper Webiro Wasira aka Wakazi ni mtu na binamu yake?
Baada ya kubaini mazungumzo yao kwenye Twitter yalionesha kuwa na uhusiano wa karibu, tumeamua kumuuliza Wakazi, yeye na Jide wakoje!!

“Jaydee ni mtoto wa baba yangu mkubwa. Anaanza baba yake Jide, anafuata baba mkubwa aliyefariki juzi halafu anafuatia baba yangu , mimi na Esther halafu anafuatia Mheshimiwa Steven Wasira,”

Wakazi ameiambia Bongo5.
Source: Bongo5.com
 
Last edited:
Picha wengine hatumjui huyo wakazi
Huyo dogo ni mnyamwezi Chikago huwa anaingia na kutoka kama nyumbani kwake wanasema ana makazi mawili mbele na hapa bongo pande za ukonga, Pia anasema mwenyewe ameshawahi kufanya kazi katika moja ya hotel za Trump huko Chikago. Yeye anafanya mziki wa hiphop just for funny maana katika maisha ameshapata ambacho wanamziki wa bongo wanakitafuta
 
Kuna mmoja umemtaja hapo katiyao, huwa namfananisha sura na kifaru.... tehteehhh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…