Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Laini za Uwakala zinasajiliwa kwa majina mahususi ya aliyeomba. Na ataendelea kutambulika kama mmiliki halali wa line hizo.Kwa wenye uzoefu,
Hivi kuna usalama kiasi ganj kununua laini za uwakala kwa mkononi mwa mtu?
Kama tayari una TIN kwaajili ya biashara nyingine kuna ulazima wa kuapply TIN mpya kwaajili ya uwakala?Airtel Money unaweza kuipata line yao kwa siku moja tu! Kwa nini usisajili biashara yako ili upate Tin pamoja na leseni ya biashara, na hivyo kupata line zenye majina yako?
TIN hiyo moja inatosha kwa kila kitu Mkuu. Leseni ya biashara yako hiyo hiyo itumie kuombea Uwakala.Kama tayari una TIN kwaajili ya biashara nyingine kuna ulazima wa kuapply TIN mpya kwaajili ya uwakala?
Hela Huwa inatolewa tu hiyo namba 1 hauko sahihi, ambacho hakiwezekani ni kui renew lakini ya uwakala sababu unakuwa huna viambata ila kama laini imepotea na Kuna Hela, hela inatolewa simple tu.Laini za Uwakala zinasajiliwa kwa majina mahususi ya aliyeomba. Na ataendelea kutambulika kama mmiliki halali wa line hizo.
Hasara zake ni zipi?
1. Ukiipoteza, omba isiwe na hela. Kama ipo nayo, atakayeweza kuirejesha ni mwenye nayo tu (mmiliki). Bahati mbaya sana mnanunua kwa madalali, ambao nao wamenunua kwa wengine, hivyo hata mmiliki halali hujawahi kumjua. Maana yake umepata hasara ya jumla.
2. Ukitaka taarifa za miamala (statements) huwezi kuipata. Mhusika pekee ndiye anaweza kwenda kuiomba. Mambo yako mengi juu ya ufuatiliaji yatashindwa kufanikiwa.
3. Endapo kuna utapeli au wizi unefanyika na bahati mbaya sana umefanyikia kwenye line yako ya Uwakala, basi uchunguzi huanzia kwako. Upelelezi huanza kwa kujua kama wewe ndiye mmiliki halali wa Till husika. Si majina wala taraafa za mmiliki unayo. Utakuwa kama sehemu ya wizi na Utapeli. Mpaka ukweli uje kufahamika umeshaumia.
4. Unavunja sheria za umiliki. TCRA na Mtandao wako wanaweza kukuwajibisha kutumia line ambayo si mmiliki halali. Wanaweza pia kukufungia watakapojisikia na hata kufreeze kiasi cha pesa kilichomo.
5. Line zingine zina mikopo mfano WEZESHA, nk. Unaweza kuchukua line, ile unaweka tu fedha wanaipitia. Aliyekuuzia atakukana. Ukiamua kwenda polisi utaambulia patupu. Unamilikije line isiyo yako?
6. Huweza kutokea mtandao wakataka kuhuisha taarifa za Uwakala. Utapaswa kufika na documents zako za line husika. Wewe huna, wanaiblock kufanya miamala.
FAIDA:
1. Utaweza kujiingizia kipato kwa kupata Commission.
2. Utakwepa msururu wa taratibu za kupata line husika.
3. Kama mmiliki alikuwa na historia nzuri, basi inakuongezea credi point za kukopesheka.
Amua kwa busara.
Wakala mkuu wa eneo lako la kazi anaweza kuhamisha Hela kwenye account ya wakala hata kama laini hiyo haipo.Kwa njia gani?
nakumbuka kuna kipindi nilisajili laini kwa wakala kumbe alifanya uhuni wa kusajili namba mbili.Hasara za hizo line ni kama muhusika anadaiwa wezesha au songesha au akaamua kukuibia hela yako kwa njia ya kwenda kurenew line. ....cha muhimu nii kusajili line yenye majina yako
Hii ni elimu nzuriLaini za Uwakala zinasajiliwa kwa majina mahususi ya aliyeomba. Na ataendelea kutambulika kama mmiliki halali wa line hizo.
Hasara zake ni zipi?
1. Ukiipoteza, omba isiwe na hela. Kama ipo nayo, atakayeweza kuirejesha ni mwenye nayo tu (mmiliki). Bahati mbaya sana mnanunua kwa madalali, ambao nao wamenunua kwa wengine, hivyo hata mmiliki halali hujawahi kumjua. Maana yake umepata hasara ya jumla.
2. Ukitaka taarifa za miamala (statements) huwezi kuipata. Mhusika pekee ndiye anaweza kwenda kuiomba. Mambo yako mengi juu ya ufuatiliaji yatashindwa kufanikiwa.
3. Endapo kuna utapeli au wizi unefanyika na bahati mbaya sana umefanyikia kwenye line yako ya Uwakala, basi uchunguzi huanzia kwako. Upelelezi huanza kwa kujua kama wewe ndiye mmiliki halali wa Till husika. Si majina wala taraafa za mmiliki unayo. Utakuwa kama sehemu ya wizi na Utapeli. Mpaka ukweli uje kufahamika umeshaumia.
4. Unavunja sheria za umiliki. TCRA na Mtandao wako wanaweza kukuwajibisha kutumia line ambayo si mmiliki halali. Wanaweza pia kukufungia watakapojisikia na hata kufreeze kiasi cha pesa kilichomo.
5. Line zingine zina mikopo mfano WEZESHA, nk. Unaweza kuchukua line, ile unaweka tu fedha wanaipitia. Aliyekuuzia atakukana. Ukiamua kwenda polisi utaambulia patupu. Unamilikije line isiyo yako?
6. Huweza kutokea mtandao wakataka kuhuisha taarifa za Uwakala. Utapaswa kufika na documents zako za line husika. Wewe huna, wanaiblock kufanya miamala.
FAIDA:
1. Utaweza kujiingizia kipato kwa kupata Commission.
2. Utakwepa msururu wa taratibu za kupata line husika.
3. Kama mmiliki alikuwa na historia nzuri, basi inakuongezea credi point za kukopesheka.
Amua kwa busara.
Hivi kupata leseni ya biashara inaweza kuchukua muda gani? MaxmumTIN hiyo moja inatosha kwa kila kitu Mkuu. Leseni ya biashara yako hiyo hiyo itumie kuombea Uwakala.