Ndiyo inawezekana kuishtaki serikali lakini kwa mazingira uliyoyasema hapo juu haiwezekani.
Ngoja niseme kwanini
Mtu anaweza kufungua shauri dhidi ya serikali kwa haki zilizopo Ibara ya 12 mpaka 29 tu. Sasa ni kwa bahati mbaya haki ya kupata huduma bora kiafya haipo katika katiba yetu ya 1977.
Pia marekebisho ya sheria ya haki na wajibu sura ya 4 na marejeo yake inamtaka mtu atakaye fungua kesi dhidi ya serikali kusema kwamba haki yake imevunjwa lazima aonyeshe, kuvunjwa kwa haki hiyo kumemuumiza vipi binafsi.
NB: serikali kutoa huduma za kijamii kama afya kunategemeana na uwezo wake huwezi kuilazimisha serikali kununua chanjo ya korona wakati haina hiyo budget na haipo kwenye vipaumbele vyake.