Njalamatata
JF-Expert Member
- Jul 12, 2010
- 293
- 154
Kagame ambaye ni rais wa RWANDA,mara nyingi mbele ya mataifa amejinasibu kuwa ni mwenye kuleta umoja kwa wanyarwanda ili kuwasahaulisha makovu ya mauaji ya kimbari.Ninaomba kufahamishwa,hivi katika baraza la mawaziri la Kagame,kuna mwaziri au makatibu kutoka kabila la wahutu? Au katika vyombo vingine vya kiutawala kama mahakama na Jeshi ? Kama wapo ni kwa ratio gani,kwa kutumia wingi wa watu,usomi au matokeo ya kibunge? Mods kama kuna thread kama hii kabla,mnaweza kuiunganisha nayo