GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Nilifika mpakani mwa Tanzania na Rwanda - Rusumo, Jana Usiku!
Baada ya kuzunguka kidogo kwa ajili ya kutafuta pa kulala, niliamua kumwuliza mtu mmoja anioneshe gesti iliyopo karibu. Aliniponipeleka alikopaita gesti, japo nilimshukuru lakini sikukubali kulala hapo! Kwa nini?
1. Tulikutana na mhudumu wa hiyo gesti akiwa nje ya geti la "gesti", lakini gesti yenyewe haikuwa na bango!
2. Nilipotaka nione kwanza chumba kabla ya kukilipia alikataa. Sina uhakika kama alinielewa kwa sababu alikuwa akijibu kwa lugha nisiyoilewa. Hakuwa akiongea Kiswahili. Walikuwa wakizingumza kilugha na huyo aliyenipeleka hapo.
3. Kutokana na hilo, niliamua kuaga na kuondoka. Nilipofika barabarani, nilimwambia boda boda anipeleke gesti iliyopo jirani.
4. Mhudumu wa "gesti" niliyoikwepa alikuwa ni mwanamke mweupe wastani mwenye umri zaidi ya miaka kumi na nane lakini chini ya miaka thelathini, kulingana na mwonekano wake. Angelikuwa "kikongwe", nisingeshangaa sana kwa yeye kutokujua Kiswahili. Najua watu wa aina hiyo, hasa wazee, wangalipo Tanzania.
Inawezekana huyo "mhudumu" hakuwa Mtanzania?