Hivi kusudi la maisha ni nini?


Kutegemea na definition yako ya kusudi, ambayo inaweza kuwa tofauti na ya mwingine, maisha hayana kusudi, ila wewe ndiyo unaweza kuyapa maisha yako kusudi.

Mfano, Nelson Mandela alivuozaliwa maisha yake hayakuwa na kusudi. Ila yeye alivyoishi aliona watu wake wanaonewa na kukandamizwa na utawala wa kibaguzi wa makaburu. Akafanya hoja ya kuuondoa utawala huu wa kibaguzi juwa ndiyo kusudi la naisha yake. Akalipa gharama kubwa sana ikiwamo kufungwa miaka mingi sana, lakini mwishowe alikamikisha kusudi lake hilo.

Sasa hivi nasoma kitabu cha mwanafalsafa maarufu wa Ufaransa mwenye asili ya Algeria aliyeshinda nishani ya Nobel katika literature mwaka 1957, anaitwa Albert Camus. Kitabu chake kinaitwa "The Myth of Sysiphus and Other Essays". Anaongelea suala hili kwa kina kikubwa.

Kitabu kingine kinachozungumzia kwa kina hoja hizi ni cha David Benatar "The Human Predicament : A Candid Guide to Life's Biggest Questions"
 
Ishi enjoy, hakuna tatizo.
 


Kushindwa kuelewa ndio kusudi namba Moja.
Unachotakiwa kujiuliza sio kusudi la maisja na aliyeumba anakusudi gani. Bali jiulize unataka uishi kwa kusudi lipi.

Tengeneza kusudi lako achana na la wengine
 
Ata duniani kila nchi ina katiba yake Raia tuifuate ukienda kinyume utaadhibiwa sasa kma binadamu tu tunafanyiana hivi je vipi kwa yule alietuumba?
Hapo kukujibu mpaka niwe kwenye hizo imani zako tofauti na hapo tupo tofauti mno , kitu mnakosea ni ku judge kila kitu na kwa kila mtu kwa misingi ya imani yako , binafsi mimi sivutiwi na kwenda huko peponi sasa hapo utani hukumu vipi kwa imani yako?
 
Ata duniani kila nchi ina katiba yake Raia tuifuate ukienda kinyume utaadhibiwa sasa kma binadamu tu tunafanyiana hivi je vipi kwa yule alietuumba?
Sasa aliyetuumba tumemkosea nini surely
Maana kama kuzini unamuumiza mpenzi wako, ukiiba unamuumiza uliyemwibia, ukiua unamuumiza aliyekuwa anampenda huyo uliyemuua, ukimpiga mtu unamuumiza huyo uliyempiga

Haya yote Mungu yanamuhusu nini? Kama yanamuumiza kwa nini haingilii kati kuzuia yasitokee? Eti anangoja ufe ndio akuchome 🤔
 
Hili nakubaliana nalo, maisha hayana kusudi ila sisi tunaweza kuyapa maisha yetu kusudi
Inabidi nianze kusoma vitabu, maana ukitoa vitabu vya darasani sijawahi kusoma kitabu kinachohusu vitu ambavyo nina interest navyo
 
Duniani tunahukumiana hpa hpa ila kwa Mungu nae ana taratibu zake kwaio usifananishe taratibu za Duniani na za Mungu
 
Duniani tunahukumiana hpa hpa ila kwa Mungu nae ana taratibu zake kwaio usifananishe taratibu za Duniani na za Mungu
Aisee. Mungu si anipe hata ishara moja tu ambayo iko direct ili niamini kuwa tunapaswa kumwabudu 😔
Huwa sielewi wanyama wengine anawaacha waishi wanavyotaka ila sisi binadamu tu ndio anataka tumuabudu na isitoshe anatuchoma tusipomwabudu. Not fair
 
Na hizo ahadi zake za wanawake wengi peponi sio kila mtu anavutiwa nazo
 
Hili nakubaliana nalo, maisha hayana kusudi ila sisi tunaweza kuyapa maisha yetu kusudi
Inabidi nianze kusoma vitabu, maana ukitoa vitabu vya darasani sijawahi kusoma kitabu kinachohusu vitu ambavyo nina interest navyo
Nimekuwekea hivi vitabu viwili hapa.

Ni vitabu vizito kifalsafa.
 

Attachments

Na tukaekewa kifo sasa mda wowote ule ili ajulikane anotenda mema ni nani na mbaya ni nani
 
Safi nakazia

Tunafanya ibada ili iweje tunamuimbia ili iweje yani vyote ili iweje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…