Tumainiandy
JF-Expert Member
- Jul 25, 2014
- 430
- 91
Napenda kuishukuru serikali kwa kujaribu kufikiri jinsi ya kutatua tatizo la msongamano ila kuna mambo ambayo ukiwa unapita unajiuliza kweli wataalamu wetu mwisho wao wa kufikiri ni hapa au,kwanza sehemu ambayo inafoleni ni kutoka Mbezi mpaka Kimara mwisho ambako kuna barabara mbili sasa unajiuliza kwanini mradi huu hakufika hata mpaka Kibaha?
Unakuwa hupati jibu ila cha kushangaza kuanzia hapo idara ya maji kuelekea mpaka Kimara barabara ya zamani ni nyembamba sana kiasi kwamba yakiwepo na hayo magari ya mwendo kasi kuna uwezekano wa kuwa na ajali yaani magari makubwa mawili hayawezi kwenda kwa pamoja hata wakoloni waliojenga barabara miaka ya 50 wanatushinda kweli.
Na ingekuwa kwa manufaa ya taifa kama zingeweka line tatu tatu kwanza ingepunguza gharama na kushughulikia tatizo la msongamano wa magari walau kwa miaka kumi ijayo lakini hapa tatizo litabaki pale pale na tumetumia fedha nyingi. Tafadhali naomba tufikirie nje ya box kwa maendeleo ya nchi yetu inauma tena inauma sana.