Itasemaje wakati mgombea urais wao ni kiongozi wa mafisadi? JK atasemaje atajipiga vita yeye mwenyewe. Sana sana baadhi ya maeneo anawadanganya wananchi kuwa wameshughulikia mafisadi na wahujumu uchumi, kwa mfano Lowasa na Mramba, wananchi walipiga makofi.
Alipoenda Rombo aliwaambia Warombo kuwa Mramba ni mtu safi, kesi dhidi yake ni 'geresha tu', wananchi walishusha makofi. Vivyo hivyo alivyoenda Monduli alisema Lowasa ni mtu safi, alionewa tu. Wananchi walipiga makofi.
Hiyo ndiyo CCM na kampeni zake, kama unasubiri waseme itapiga vita ufisadi, rushwa na uhujumu uchumi, subiri.
Lakini katika yote kwa mtazamo wangu wa kulaumiwa ni wananchi wanaopiga makofi ovyo hata wakitukanwa. Sielewi tatizo ni unafiki au woga.
Kwa mwanchi anayefikiri vizuri, asiye mnafiki wala mwoga, Kikwete kusema kuwa Lowasa na Mramba walionewa, ni watu safi ni matusi. Walitakiwa wamzomee Jk na kumwacha uwanjani apige blaablaa zake.
NAWAPONGEZA WANANCHI WA MBULU WALIOMZOMEA Kikwete na kuanza kuondoka alipoanza kuzungumza ubaya wa vyama vya upinzani. Hao ni wazalendo wasio na unafiki na woga.
Kwa mtaji wa woga na unafiki uliooneshwa na Warombo na wamonduli, ambao pia unaendelea kuoneshwa sehemu mbalimbali kampeni zinapoendelea hatufiki, wala tusilalamike tunapopokonywa haki zetu.