CAMARADERIE.
Nyumbani kwako kukoje?
Nyumb nayo inahitaji kuwa na katiba kama nchi............nyumba nyingi hazina katiba au kama ipo ni page mbili tu....katiba yangu kama ya nchi kwa hiyo hakuna masikhara....weka appointment uje utembee mkuu ujionee
Isije kuwa Katiba ya nyumbani kwako kama ya Tanzania inakanyagwa hovyo tu..inaitaji marekebisho kibao
Hapana ilitungwa kwa ushiriki wa wote baba,mama na watoto....wageni wakija wanasomewa riot act......mambo yanaenda vizuri kipengele muhimu.......'' Baba kamwe asionekana kuwa amechelewa kurudi nyumbani,muda wowote atakao rudi atakuwa amewahi hata kama ni asubuhi''
Vipi kipengele cha wa watoto, mtoto wa kike anaruhisiwa kuleta rafiki yake wa kiume nyumbani kwako?
Katika haki zake za msingi za Katiba inavyomlinda akirudi usiku kutoka club unamfungulia mlango, kulinda Katiba ya nyumbani
Almradi awe amevuka miaka 21 anaweza kwenda out at will........kuleta kijana ni mpaka atakapokuwa tayari kuolewa........wakiume marufuku kula house girl
Mkuu, Katiba yako mbona ya kibaguzi sana inaitaji marekebisho makubwa..
Mtoto wa kiume haki zake za msingi zimeminywa kwa makusudi..
Hapo ndio unataka iwe legelege
Kwa style yako mkuu, lazima mtoto wa kike hatakuwa mwenye sauti nyumbani..
Na mtoto wa kiume unamjenga aje kuwa baba wa nyumbani tu
Wewe katiba yako iko wapi kabla hujamtuhumu mwenziyo
Wanaume wengi wamewekwa ndani tu kwa ajili ya kuwaridhisha kimwili, lakini wanawake ndio wanaomiliki fedha, magari , nyumba n.k hapo unategemea sauti itatoka wapi?
sikuhisi wanawake wanawaletea kibess wanaume sababu ya limbwata.mia
Kuna jamaa yangu mmoja wife wake kampiga marufuku kutembea hovyo baada ya kazi..
Ukipita nyumbani kwake jioni jamaa kakaa nje na watoto wife hayupo..
Nilichokigundua hapa ni kwamba wewe ni mbea, mchonganishi na hupendi kuona watu wanaelewana katika ndoa zao. Pia nina wasiwasi huyo jamaa alikuwa anakutwanga ofa za bia wakati yupo free....sasa kitendo cha kupigwa marufuku na wife wake kutoka kimekuathiri na wewe, pole sana kama sio kweli!
Dada yangu utakuwa unakaa Tandale kwa Tumbo sio bure..
Great Thinkers hatuna watu wa namna yako..lol..hapa tunajadili kwa upendo na amani, nilichogundua JF hapakufahi rudi FB...lol
Sawa Dada yangu nakubaliana na wewe yote uliosema, sisi wengine JF ni Furaha tupu..kama thread yangu imekukwaza nisamehe dada yangu sirudii tenaNi wapi wanapokaa Great thinkers? Wahenga walisema, "Ukweli unauma"