Inatokea unakutana na posti ya maana tu tena kwenye page ya Mtu wa heshima, ila unapoenda upande wa comment unakutana na comment isiyohusiana kabisa na kilichopostiwa na mbaya zaidi ni comment ya matusi.
Hivi Mwenye page haoni kama hilo linawakwaza wale wanaomfuata? Hawana namna ya kuziondoa?
Nilidhani Mwenye page ndiye alipaswa kuhakikisha page zake zinabaki salama?.
Unakuta Mtu kaweka post ya maana, labda kuhusu kumchangia Mtoto Mgonjwa anayehitaji kufanyiwa upasuaji na Ndugu zake na Jamaa hawana uwezo, sasa cha ajabu unakutana na Mtu kaingiza comment isiyohusiana kabisa na taarifa iliyopo....na posti yenyewe ni ya matusi.
Inasikitisha unakuta hata page za Watu wanaofuatiliwa na Watu wengi nazo zinakuwa na haya madudu, hivi hakuna namna ya kidhibiti/kuzuia?.
Haswa kwa wenye page husika wao si huziona hizi meseji?...Je wanaona sawa kuachwa zisomwe tu na kila anayepitia page zao?.
Mtu kama Milard kwa heshima aliyojiwekea kwenye Jamii haoni ni tatizo kuacha page yake itumike kama bango la matusi ili hali akijua ya kuwa anafuatiliwa na Watu wa kila rika na hadhi?. kuna Mapadre, Masheikh, Masista n.k.