Elections 2010 Hivi kwa sasa chama 'kikuu' cha upinzani zanzibar ni kipi?

Elections 2010 Hivi kwa sasa chama 'kikuu' cha upinzani zanzibar ni kipi?

Waridi

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2008
Posts
1,025
Reaction score
172
Wakuu,
Serikali iliyotwaa madaraka kuanzia leo visiwani ni ya vyama vya CCM na CUF. Kwa hiyo chama kikuu cha upinzani Zanzibar ni kipi, Jahazi asilia?
 
CUF..........CCM ndio wameshinda!!!!
 
Hakuna chama kikuu cha upinzani....ni Zimbabwe-Kenya style!
 
Hakuna chama cha upinzani zanzibar ila kuna chama kimoja kinaitwa mwafaka ndio chama twawala.
 
Wakuu,
Serikali iliyotwaa madaraka kuanzia leo visiwani ni ya vyama vya CCM na CUF. Kwa hiyo chama kikuu cha upinzani Zanzibar ni kipi, Jahazi asilia?

Kama kuna chama ambacho kimepata nafasi ya uwakilishi zaidi ya CCM na CUF basi hicho chama ndio kitakachokuwa cha upinzani.
Labda swali jingine ni kwamba serikali ya CCM na CUF watatekeleza sera za chama gani?
 
Demokrasia na ushindani umekufa rasmi znz tangu mwafaka Cuf na ccm watasaidiana kupinga upinzani. Labda chadema ikishakaa sawa kule zenji wasubiri kdogo tu!
 
NAOMBA NIWE NITAKOSEA, LAKINI MUUNGANO HUU WA CCM CUF HAUTADUMU ZAIDI YA MIAKA MIWILI - Tusubiri tuone, langu :bowl:
 
hii ni janja ya wazanzibari ili wajitoe kwenye muungano wakifanikiwa upinzani palepale
 
Back
Top Bottom