Hivi kwanini Diamond asitangazwe kama hazina ya taifa?

el nino

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2013
Posts
4,712
Reaction score
5,058
Nilisikitishwa sana baada ya kutambua kuwa pamoja na kuwa na mlima kilimanjaro, ziwa Tanganyika, migodi, mbuga na mengineyo bado kuna watu wapo hapahapa afrika lakini hawaijui wala hawajawahi kuiskia Tanzania.

Kumbukumbu zangu zinanirudisha nyuma wakati timu ya taifa ya Ivory coast ilipokuja kucheza na Tz kwa mara ya kwanza ndipo kina Drogba, yaya toure na wengineo wakaulizwa kama wanafahamu chochote kuhusu Tz wakajibu kuwa hawakuwahi hata kuiskia kabla ya kupangiwa nayo katika hatua za makundi ya kombe la mataifa afrika.

Katika kuchat kwnye mitandao ya kijamii na marafiki mbalimbali wa afrika kaskazini na magharibi nikijaribu kuwagusia kuhusu Tz wakawa wanajibu hawafahamu chochote wala lolote kuhusiana na Tanzania.

Hapo nikaanza kupata picha kuwa Tanzania sio famous kama watu wengi tunavyofikiri...mi nilitegemea ukimtajia mtu kuhusu Tz teyari anakuwa anaijua na picha ya mlima kilimanjaro imjie kichwani ...lakini la hasha kumbe nilikuwa nawaza mbali sana ndani nchi ambayo haina muda wa kupromote vitu vyake..

Katika mawazo hayo nikakumbka Mungu hakutuacha hivihivi ametupa mlima mrefu zaidi umetushinda kuutangaza ndipo akatokea msanii ambaye tukubali au tukatae anajulikana sana kwa sasa na anaitangaza vema nchi yetu zaidi hata ya hivi vivutio ambavyo vimetushinda kuvitangaza, leo hii kuna watu wanamfahamu Diamond ila hawaujui mlima Oldonyolengai, kuna watu wanamfahamu Diamond ila hawayajui madini ya Mwadui, kuna watu wanamfahamu Diamond ila hawaifahamu Tanzanite.

Miaka mingi iliyopita aliyekuwa mchezaji nguli wa Brazi "pele" alitangazwa na nchi ya Brazil kama hazina ya taifa kutokana na sababu hizohizo za kuwa alama ya utambulisho wa Taifa lake, maana kuna watu mpaka leo wanaifahamu Brazil kwaajili ya mpira tu...hawajui kuwa Brazil kuna mto na msitu wa Amazon, hawajui lile sanamu kubwa pale Rio, hawajui kuwa Brazil ni nchi inayoongoza kwa natural Resources duniani...wanaijua Brazil kwa sababu ya kina " Pele"...full stop!

Hivi kwann leo hii Tz Diamond asitangazwe kama hazina ya taifa kama alivyofanyiwa Pele na wtu wengne..maana teyari amefanya mambo na kuitambulsha nchi yetu kitu ambacho hata wakongwe kama kina Marijani rajab, Tx moshi, mtoto wa dandu, jide na wengineo hawajawahi kufanya...

Wakati naandika uzi huu Diamond amechaguliwa kwnda kutumbuiza lagos kwny utoaji wa tuzo za mchzaji bora afrika....

Hivi kwanini asitangazwe hazina ya taifa?
 
kuna madini mengi na ardhi ya kutosha.
 
hii nchi ndo maana wajanja wanapiga hela kama za escrow halafu tunapandishiwa bei ya umeme kama mawazo yenyewe ni kama ya huyu mleta mada...jinga kabisa wewe!
 
Hivi kwann asitangazwe hazina ya taifa?????????

Kwa wazo kama hili wewe mwenyewe unafaa sana kuwa kivutio cha utalii hapa nchini.....

Mana unaeza kuingia ktk list ya watu wenye uwezo mdogo sana wakufikiri.
 

Umenena vema lakini nisaidie yafuatayo

1. Vigezo vya mtu kuwa hazina ya taifa nini like how long did it take for pele kutangazwa kuwa hazina 5 years?10 years? etc ili isije ikawa fashion.

2. Nimepata bahati kidogo kuzura baadhi ya nchi za Africa na hata majuu, according to my simple observation watanzania wanaongoza duniani kwa kudadisi masuala ya kimataifa something that u cannot find anywhere. Wenzetu mtu wa let's say kariakoo hajui na wala hataki kujua kinachoendelea mlimani city.
 
Usikute na wewe una familia na wanategemea mawazo yako?! Dah! Tz tutachukua muda mrefu sana kufika kule tunakokuota km mawazo ya watu ndo haya.
 
Jamii Forums raha sana; where we dare to talk openly. Huyu jamaa ana uwezo wa kujenga hoja, ame-derive vizuri sana point yake. Nasikitika sicho tunachohitaji kama Taifa.
 
china pia wanamtumia jack chan kama kitambulisho cha taifa lao ila diamond bado sana kwasababu akuna msanii wa cameroon aliefika mbali kama AKON lakini awajafanya ivo ata ukiangalia nigeria D banj 2 face wanafanya vzuri pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…