Hivi kwanini hatuwawezi Uganda kwenye soka?

Hivi kwanini hatuwawezi Uganda kwenye soka?

May Day

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2018
Posts
6,311
Reaction score
9,027
Tangu niliposikia tumeingia fainali ya under 17 na Uganda nilijua tuna nafasi ya asilimia 30 tu za kushinda, na kweli tumebamizwa 3 na hii ni baada ya juzi juzi tena kupoteza fainali nyingine kwa hawa hawa Waganda.

Hata ile fainali ya kufuzu Afcon ni wazi tulipewa tu na Uganda kwa ujirani mwema na ukaribu wetu na Mzee Mu 7, na tukashangilia kama mazuzu...walahi kama ile ingekuwa ni mechi ya mmoja lazima ashinde aende tungebamizwa tu.
 
Wachezaji wanaonekana hajafundishwa mbinu za uchezaji:kipiga pasi,kukaba,kulinda na ujanja wa kufungua nafasi.
Udhaifu unaonekana wazi,maswali yanakuja:

1. Kiwango cha ufundishaji na aina ya Mwalimu.

2. Aina ya wachezaji na aina ya mafunzo waliyopata.

3. Uwezo binafsi wa wachezaji wetu.

Kuna baadhi ya misingi inakosekana kwa timu na taaluma.
 
Tangu niliposikia tumeingia fainali ya under 17 na Uganda nilijua tuna nafasi ya asilimia 30 tu za kushinda, na kweli tumebamizwa 3 na hii ni baada ya juzi juzi tena kupoteza fainali nyingine kwa hawa hawa Waganda...
Soka letu lina uccm mwingi sana, matokeo yake tunaua vipaji badala ya kuvikuza, siku tukiondoa uccm kwenye soka letu tutafika mbali sana, maana tunavipaji vingi sana.
 
Tatizo kubwa lililopo mkuu ni uwekezaji tu hamna mchawi mwingine zaidi ya huyu! Saivi kinachofanyika ni connection kuunda hizo timu zw vijana, kuna kipindi aliletwa kocha mzuri sana kutoka nje sijui alikuwa anaitwa poulsen yule if am not mistaken, matokeo yake akaundiwa zengwe akatimliwa!

Upuuzi mtupu unaoendelea nchi hii, connection zimekuwa nyingi wakati kuna vipaji vipo vikubwa sana hapa kwetu!

Tukiwekeza kwenye mpira tunaeza fika mbali
 
Wachezaji wanaonekana hajafundishwa mbinu za uchezaji:kipiga pasi,kukaba,kulinda na ujanja wa kufungua nafasi.
Udhaifu unaonekana wazi,maswali yanakuja:
...
Wenzetu Waganda wao wanafundishwa na nani?
 
Tatizo kubwa lililopo mkuu ni uwekezaji tu hamna mchawi mwingine zaidi ya huyu!...
Ni kama naipata vizuri pointi yako.

Na hii kansa tunayo kwenye maeneo mengi sana haswa yanayohusisha vipaji.

Mfano unaweza kusikia tu taarifa kwamba kuna Vijana/Watu wametuwakilisha kwenye mashindano ya sanaa fulani nje ya nchi na wala hujui hao wawakilishi wamepatikana vipi...yaani hujasikia wito wowote wa kimkoa wala kitaifa Watu wakachujwa.

Kama mfano kuna wakati miaka kadhaa nyuma nasoma mtandaoni eti Msanii fulani yupo Marekani anawakilisha nchi kwenye siku ya Kiswahili au tamasha la kiswahi kama sijakosea, ili hali huyo Msanii hata kuongea Kiswahili hajui..akiambiwa taja Mikoa iliyopo Tanzania atakwambia Lukwa, Luvuma, Mala, Alusha..achilia mbali hicho kiingereza anachokwambia "nime msplaiz".
 
Soka letu lina uccm mwingi sana, matokeo yake tunaua vipaji badala ya kuvikuza, siku tukiondoa uccm kwenye soka letu tutafika mbali sana, maana tunavipaji vingi sana.
Mkuu hii mbona umeiweka kisiasa sana.
 
Wenzetu wana mfumo mzuri wa kuandaa wachezaji wa vijana na upatikanaji wa makocha tofauti na sisi kocha anachukuliwa yuko kijiweni
 
Bongo siasa nyingi sana yan hata kuchaguliwa hizi team za taifa ni siasa tu,hawaangalii vipaji wala nni ukweli ni kwamba kuna wachezaji wengi ktaaa wanavpaji katika soccer bt njia ya kufika huko juu ndo wamekaa hawa wapga madili.
 
Tangu niliposikia tumeingia fainali ya under 17 na Uganda nilijua tuna nafasi ya asilimia 30 tu za kushinda, na kweli tumebamizwa 3 na hii ni baada ya juzi juzi tena kupoteza fainali nyingine kwa hawa hawa Waganda.

Hata ile fainali ya kufuzu Afcon ni wazi tulipewa tu na Uganda kwa ujirani mwema na ukaribu wetu na Mzee Mu 7, na tukashangilia kama mazuzu...walahi kama ile ingekuwa ni mechi ya mmoja lazima ashinde aende tungebamizwa tu.
Ile AFCON nakataa kwakuwa hata match ya kwanza iliyofanyika Uganda hakuna aliyekuwa amefudhu. Kumbuka ile game ya kwanza ilitoka bilabila. Kipindi cha kwanza Waganda walicheza poa but kipindi cha pili Waganda walipotezwa sana na Samatta angeongeza umakini walikuwa wanakufa 2 wale. Match ya pili ilikuwa lazima Uganda afe.
 
Tatizo linaanzia hapa.

Baada ya hayo mashindano kuisha watafute hao wachezaji kama utawapata..kila michuano tunaanza upya maandalizi ya zima moto baada ya mashindano kila mtu na 50 zake
 
Back
Top Bottom