Hivi kwanini matajiri wengi huwa na urafiki na matajiri wenzao tu

Cute Cindy

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2019
Posts
211
Reaction score
594
Hii hali nimeiona Kwa watu wengi waliofanikiwa kiuchumi, huwezi kuta tajiri ana mazoea ya karibu na msukuma mkokoteni, yani tajiri huwa ana-socialize na matajiri wenzake tu, nyie wenyewe mnaweza kuwa mashahidi.

Hiyo hali Inasababishwa na nini? Nyodo, kutojiamini, kiburi au
 
Ukikaa sana na masikini siku zako za kuwa masikini zinahesabika. Maana utajihisi wewe ndio biligate kwa sifa lukuki wakupazo. Ogopa sana mkuu kukaa na mtu usiyefanana nae maana wao cha muhimu salamu kwanza usipowasalimia unajidai kwa kuwa unazo hata kama uwe na stress yaaani ni shida. Kila siku huisi mtu wa kuonewa tu
 
Utajiri ni mafanikio na katika kanuni za mafanikio ni pamoja na kua karibu na watu waliofanikiwa (urafiki).
Kwahiyo kuanzia leo ww ukitaka kua mtunzi wa vitabu mahiri tafuta urafiki na watunzi bora wa vitabu.Ukitaka kua mwanasheria mahiri tafuta urafiki na wanasheria bora kabisa.n.k

Kwahiyo matajiri wanatengeneza urafiki kati yao kwa sababu ndivyo inavyokuza utajiri wa kila mmoja wao.
 
Swala atakuwa rafiki wa swala
chui atakuwa rafiki wa chui
haitakaa itokee swala akawa na urafiki na chui
 
Hii hali nimeiona Kwa watu wengi waliofanikiwa kiuchumi, huwezi kuta tajiri ana mazoea ya karibu na msukuma mkokoteni, yani tajiri huwa ana-socialize na matajiri wenzake tu, nyie wenyewe mnaweza kuwa mashahidi.

Hiyo hali Inasababishwa na nini? Nyodo, kutojiamini, kiburi au
Sasa wewe choka mbaya utampa mawazo gani zaidi ya kupiga vibomu na kumpa sifa za kijinga akikaa na matajiri wenzie watapena maujanja ya hapa na pale kwa kweli nauchukia sana umakini sema basi tu naukimbia kama chui
 
Ukikaa sana na masikini siku zako za kuwa masikini zinahesabika. Maana utajihisi wewe ndio biligate kwa sifa lukuki wakupazo. Ogopa sana mkuu kukaa na mtu usiyefanana nae maana wao cha muhimu salamu kwanza usipowasalimia unajidai kwa kuwa unazo hata kama uwe na stress yaaani ni shida. Kila siku huisi mtu wa kuonewa tu
Hii Ina ukweli sana na nimeishuhudia kwenye mitaa ninayoishi ingawa Mimi sio tajiri kipesa ila ni tajiri wa kifikra.
Utakuta mtu una stress zako wanaanza kukukasirikia from nowhere au wanataka ukipita barabarani kwenda nyumbani kwako unsalimie kila mtu,yaani hata waliopo nyumbani kwao wote uwasalimie hata Kama wapo umbali wa mita 150 kutoka barabarani.
Usipofanya hivyo wanaanza kukusema vibaya na kukujadili.
Kiukweli watu maskini Wana muda mwingi sana wa kupoteza.
 
Hii hali nimeiona Kwa watu wengi waliofanikiwa kiuchumi, huwezi kuta tajiri ana mazoea ya karibu na msukuma mkokoteni, yani tajiri huwa ana-socialize na matajiri wenzake tu, nyie wenyewe mnaweza kuwa mashahidi.

Hiyo hali Inasababishwa na nini? Nyodo, kutojiamini, kiburi au
Sasa mtu tajiri akae na maskini kujadili labda biashara ya kufanya kwa mtaji wa milioni 300 huyo maskini si ataona kama anadhihakiwa, kwanza utakuwa mwanzo wa kurogwa su kutumiwa majambazi.
 
Hii hali nimeiona Kwa watu wengi waliofanikiwa kiuchumi, huwezi kuta tajiri ana mazoea ya karibu na msukuma mkokoteni, yani tajiri huwa ana-socialize na matajiri wenzake tu, nyie wenyewe mnaweza kuwa mashahidi.

Hiyo hali Inasababishwa na nini? Nyodo, kutojiamini, kiburi au
Chemchem haitiririki jangwani itakauka
NB : sio jangwani ya [emoji196] FC
 
Back
Top Bottom