Hivi kwanini Serikali inashindwa kuwaendesha EWURA?

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2020
Posts
7,899
Reaction score
10,415
Hivi ni sababu zipi zinazofanya Serikali ishindwe kuwaendesha EWURA?

Kwasababu naona kila kitu wanajipangia wao tu.

1. Bei za mafuta wanajipangia wao tu watakavyo
2. Kuajiri wanajiajiria wenyewe tu wao wala hawataki utumishi iajiri badala ya wao

Kuna nini hapo.

Jamani Mh. Rais Samia litazame hili kwa undani.
 
..ewura kama mamlaka ya udhibiti haitakiwi kuingiliwa na serikali ktk kutekeleza majukumu yake.

..wana taratibu zao za kufuata mpaka kufikia maamuzi ya kupandisha au kuteremsha bei ya bidhaa au huduma wanazosimamia.

..serikali inaweza kuwa-challenge ewura kama watakuwa wamekiuka sheria au taratibu zinazotakiwa kufuatwa ktk kufikia maamuzi na kutekeleza majukumu yao.
 
Inakuwaje Serikali inakataa bei ya EWURA ?

Ina maana Wizara husika na EWURA hamna mawasiliano kabla hamjaja public?.wote si ni Serikali?.
 
..ewura kama mamlaka ya udhibiti haitakiwi kuingiliwa na serikali ktk kutekeleza majukumu yake.

..wana taratibu zao za kufuata mpaka kufikia maamuzi ya kupandisha au kuteremsha bei ya bidhaa au huduma wanazosimamia.

..serikali inaweza kuwa-challenge ewura kama watakuwa wamekiuka sheria au taratibu zinazotakiwa kufuatwa ktk kufikia maamuzi na kutekeleza majukumu yao.
Why cant they discuss and be challenged kabla ya kuja public?

kama hawaingiliwi mbona Serikali imewadindia?.
 
Hivi ni sababu zipi zinazofanya serikali ishindwe kuwaendesha EWURA??

Kwasababu naona kila kitu wanajipangia wao tu.

1. Bei za mafuta wanajipangia wao tu watakavyo.
2. Kuajiri wanajiajiria wenyewe tu wao wala hawataki utumishi iajiri badala ya wao.

Kuna nini hapo.
Jamani Mh. Rais Samia litazame hili kwa undani.
Hata mimi nashangaa kwamba Ewura kila wanachotaka kufanya huwa hawalazimiki kupata approval ya Wizara ya Nishati au huwa wanatufanyia maigizo baada ya kupima upepo?
 
Hivi kipindi cha jiwe mafuta yalisimama chini ya buku mbili ila kwa sasa naona yatafika 5000 lita ni jambo la mda tu maana wauza mafuta sio watu wazuri soko likipungua ni wagumu sana kupunguza.
 
Why cant they discuss and be challenged kabla ya kuja public?

kama hawaingiliwi mbona Serikali imewadindia?.

..katika mfumo wa soko huria serikali haitakiwi kuwa ni mpangaji wa bei za bidhaa na huduma.

..badala yake mamlaka za udhibiti wa bidhaa na huduma ndizo zenye jukumu hilo kisheria.

..tatizo lililopo ni serikali kutokufuata sheria na kuingilia majukumu ya ewura pamoja na mamlaka nyingine za udhibiti.

..watendaji wa ewura nao huwa wananywea kwasababu wanajua kwamba serikali ya Tz iko juu ya sheria. serikali ikiamua jambo lake hakuna mahakama au chombo chochote kinachoweza kuamua kwa haki.
 
..katika mfumo wa soko huria serikali haitakiwi kuwa ni mpangaji wa bei za bidhaa na huduma.

..badala yake mamlaka za udhibiti wa bidhaa na huduma ndizo zenye jukumu hilo kisheria.

..tatizo lililopo ni serikali kutokufuata sheria na kuingilia majukumu ya ewura pamoja na mamlaka nyingine za udhibiti.

..watendaji wa ewura nao huwa wananywea kwasababu wanajua kwamba serikali iko juu ya sheria. serikali ikiamua jambo lake hakuna mahakama au chombo chochote kinachoweza kuamua kwa haki.
Hatukatai mandate ya EWURA na uwezo wa Serikali
My point is public optics

EWURA anatangaza Waziri anapiga stop
Hawakujadiliana?hakujua?ni nini hiki?.serikali haina coordination ama?.

tumlaumu nani?.
 
Hata mimi nashangaa kwamba Ewura kila wanachotaka kufanya huwa hawalazimiki kupata approval ya Wizara ya Nishati au huwa wanatufanyia maigizo baada ya kupima upepo?

..sheria inaelekeza wafanye maamuzi bila kushawishiwa au kushinikizwa na wizara au serikali.

..pia ewura ni mamlaka iliyoko chini ya wizara ya maji, haiko chini ya wizara ya nishati.

..ewura ni Energy and Water Utilities Regulatory Authority, bunge ndilo lilipitisha sheria wawe chini ya Wizara ya maji.
 
Hatukatai mandate ya EWURA na uwezo wa Serikali
My point is public optics

EWURA anatangaza Waziri anapiga stop
Hawakujadiliana?hakujua?ni nini hiki?.serikali haina coordination ama?.

tumlaumu nani?.

..nadhani ni waziri anatafuta kiki.
 
Hiyo kitu mi sioni umuhimu wake, kama serikali imeingilia Kati ina maana Hawa a umuhimu waivunje tu. Unajua hutu ni tumamlaka tulitokuwa tunaanzishwa kiushkaji sasa nashangaa eti akataki kuingiliwa? Kameota mapembe!
 
Ewura inatakiwa iwe ni Wakala chini ya Wizara ya Fedha au /Viwanja na Biashara.
Uthibiti wa Ewura ni Price Control kwenye huduma za Nishati na Maji ,hata hivyo wanaweza kuongeza na Wakala wa vipimo wakawa under One Roof.
 
Hii EWURA wamrudishe yule mkurugenzi aliyesimamishwaga na PM.Bwana Felix Ngamlagosi naimani atatusaidia Sana.Maana Mpaka sasa Toka aondoke imepwaya Sana.
 
EWURA ni mamlaka, haipaswi kuingiliwa na serikali kwenye kutimiza majukumu yake.

Swali ni je? Hawana justification za kupandisha bei? Kama wanayo, tatizo liko wapi? Serikali iseme ukweli, kwenye lita 1 ya mafuta kodi na tozo ni kiasi gani? Wasiwalaumu tu EWURA
 
Hii EWURA wamrudishe yule mkurugenzi aliyesimamishwaga na PM.Bwana Felix Ngamlagosi naimani atatusaidia Sana.Maana Mpaka sasa Toka aondoke imepwaya Sana.
Mkuu Taasisi sio mtu, taasisi ni mfumo jumuishi wenye mission na vision ya mbali.
Viongozi wenye ubunifu na mawazo /maono mazuri wapo.
Ili Ewura ilifanye vyema ikaribishe maoni ya wadua ili iyatumia kuboresha huduma kwa kuanzia.
 
Hakika Mmojawapo ni huyo Ngamlagosi.Enzi zake Aliweza kufanya Kazi nzuri sana.Atamsaidia Mama Yetu vyema kwenye haya mambo.
 
Back
Top Bottom