Acha kumsagia kunguni Mkurugenzi Mkuu wa sasa ambaye ni kichwa kizuri chenye elimu kutoka vyuo vikuu vikubwa vya USA [emoji631]Hii EWURA wamrudishe yule mkurugenzi aliyesimamishwaga na PM.Bwana Felix Ngamlagosi naimani atatusaidia Sana.Maana Mpaka sasa Toka aondoke imepwaya Sana.
Funguka mzee babaEWURA ni mateka inaendeshwa na mabepari wenye chenchi zao
Sent from my Infinix X692 using JamiiForums mobile app
Kwa nini alitumbuliwa? Tuanzie hapoWewe vipi?? Tunamtaka huyo FELIX, ndiye mbeba maono!!
Inakula % sokoni ..huo ndo udalali wenyewe...yaani ni serikali ya energy Tanzania...je na walimu wawe na % ktk kila school fees inayolipwa...ewura kama mamlaka ya udhibiti haitakiwi kuingiliwa na serikali ktk kutekeleza majukumu yake.
..wana taratibu zao za kufuata mpaka kufikia maamuzi ya kupandisha au kuteremsha bei ya bidhaa au huduma wanazosimamia.
..serikali inaweza kuwa-challenge ewura kama watakuwa wamekiuka sheria au taratibu zinazotakiwa kufuatwa ktk kufikia maamuzi na kutekeleza majukumu yao.
Hapo kwenye kodi na tozo kwa lita moja ndipo ilipo siri ya bei kubwa ya mafuta hapa Tz ukilinganisha na nchi za jirani kama Zambia nk. Serikali imekimbilia kukamua wenye vyombo vinavyotumia hii nishati kama vile ni vyombo vya anasa bila kufikiri kwamba kwa kufanya hivyo itasababisha mfumuko wa bei kwa bidhaa mbalimbali na kumfanya mwananchi asiweze kumudu maisha.EWURA ni mamlaka, haipaswi kuingiliwa na serikali kwenye kutimiza majukumu yake.
Swali ni je? Hawana justification za kupandisha bei? Kama wanayo, tatizo liko wapi? Serikali iseme ukweli, kwenye lita 1 ya mafuta kodi na tozo ni kiasi gani? Wasiwalaumu tu EWURA
Angalia thread humu ndani mbona Kuna Wadau waliletaKwa nini alitumbuliwa? Tuanzie hapo
Hao wote ni wasomi wazuri na walifanya Kazi kwa Pamoja.Ni Bora Felix kama ilivyoelezwa Awali ya Kuwa alisamimishwa basi Mhe.Majaliwa kama alivyokuwa amemsimamisha arudishwe aendeleze Kazi na huyo msaidizi wake ambaye ni Kaimu mkurugenzi Kwa Sasa.Acha kumsagia kunguni Mkurugenzi Mkuu wa sasa ambaye ni kichwa kizuri chenye elimu kutoka vyuo vikuu vikubwa vya USA [emoji631]
Umejibu kwa weledi na hekima sana. Acha kazi iendeleeHao wote ni wasomi wazuri na walifanya Kazi kwa Pamoja.Ni Bora Felix kama ilivyoelezwa Awali ya Kuwa alisamimishwa basi Mhe.Majaliwa kama alivyokuwa amemsimamisha arudishwe aendeleze Kazi na huyo msaidizi wake ambaye ni Kaimu mkurugenzi Kwa Sasa.
Hapa umenena hawa jamaa wamegeuza mafuta sehemu ya kuvuna pesa Kwa matumizi wanayoyataka bila kuangalia madhara yake.Hawajali mfumko wa Bei unaotokea, hawajali mabadiliko ya maisha yanayoleta umasikini zaidi.Hapo kwenye kodi na tozo kwa lita moja ndipo ilipo siri ya bei kubwa ya mafuta hapa Tz ukilinganisha na nchi za jirani kama Zambia nk. Serikali imekimbilia kukamua wenye vyombo vinavyotumia hii nishati kama vile ni vyombo vya anasa bila kufikiri kwamba kwa kufanya hivyo itasababisha mfumuko wa bei kwa bidhaa mbalimbali na kumfanya mwananchi asiweze kumudu maisha.
Baada ya upandaji mfululizo wa bei za mafuta, kilichokua kinafuata ni kupanda kwa nauli au migomo ya vyombo vya usafiri na upandaji wa bei za bidhaa au kuadimika. Hilo lingeleta mkanganyiko kwa wananchi na kusababisha kelele kwa serikali.
Katika hayo mapitio ya hivyo "viashiria vinavyosababisha" kupanda bei ya mafuta, wajikite tu kwenye huo utitiri wa kodi na tozo, hakuna cha bei ya soko la dunia wala kingine zaidi ya hapo. Zambia nao wanatumia mafuta hayo hayo yanayotoka kwenye hilo hilo soko la dunia na yanapitia kwenye bandari yetu ya Dar es Salaam.
Hakika.Nchi yetu inajengwa nasi Sote.Huyo Mzee Felix wangemrudisha tu,alipokaa nje naimani atakuwa na mawazo chanya na ataendeleza kazi alipokuwa ameishia na wenzake.Kazi iendeleeUmejibu kwa weledi na hekima sana. Acha kazi iendelee
mimi sidhani kama huyo Felix ndio mwenye uwezo kuliko watu wote Tanzania. Haya mawazo yaondoe. Tunachotaka kuona ni serikali kuindesha EWURA kwenye kazi zao sio wawe wanajipangia kila kitu.Hakika.Nchi yetu inajengwa nasi Sote.Huyo Mzee Felix wangemrudisha tu,alipokaa nje naimani atakuwa na mawazo chanya na ataendeleza kazi alipokuwa ameishia na wenzake.Kazi iendelee
Hakuna taasisi ya serikali itakuwa fully autonomous, yaani ina absolute power ya kufanya chochote, Hiyo.ni taasisi ya serikali chini ya wizara ya maji,japo kuna aspect ya Nishati.kwaakili ya kawaida kwakuwa majukumu yake ni udhibiti wa maswala nyeti yanayogusa raia moja kwa moja kama gharama za maji au nishati (mafuta,gesi,umeme etc) kuna wakati katika hali ya kawaida walitakiwa waombe muongozo katika kutoa bei mpya tena itakayozidisha ugumu wa maisha kwani watakaolaumiwa ni serikali kwa ujumla.kwa hili la juzi walichemsha kulingana na hali ilivyokuwa huku "tozo" kubwa zikilalamikiwa zishushwe,huku luku-property taxes, nk. Sasa wewe unakuja na 'nyundo' nyingine tena kali ambayo hiyo tena ndio itapandisha gharama zote za maisha.ule ungekuwa ni uchonganishi mkubwa kati ya serikali na wananchi wake as it was a very wrong timing,hata kama hesabu zinasoma hivyo,kuna maslahi zaidi ya kuangalia.
mimi sidhani kama huyo Felix ndio mwenye uwezo kuliko watu wote Tanzania. Haya mawazo yaondoe. Tunachotaka kuona ni serikali kuindesha EWURA kwenye kazi zao sio wawe wanajipangia kila kitu.
hata wewe unaweza kuwa mkurugenzi wa EWURA kwani EWURA ina nini cha ajabu basi kila mtu mwenye elimu anaweza kuwa...ewura imekuwa ikiongozwa na kaimu mkurugenzi mkuu tangu felix ngamlagosi alipo ondolewa kwa maagizo ya Waziri Mkuu Majaliwa mwaka 2017.
..nakumbuka aliondoka kutokana na mgogoro wa IPTL ku-renew leseni ya kuzalisha umeme.
..Ewura wali-renew leseni huku serikali ikiwa mbioni kuwashtaki na kuwaweka kizuizini James Rugemalira na Habinder Singh ambao ni wamiliki wa IPTL.
..Kilichofuatia hapo ni Mkurugenzi Mkuu wa Ewura kuondolewa kazini kwa maelekezo ya Waziri Mkuu. Na tangu wakati huo Ewura imekuwa ikiongozwa na kaimu mkurugenzi mkuu.