Hivi kwanini timu ndogo za ligi kuu zinapenda sana kutoka sare?

Hivi kwanini timu ndogo za ligi kuu zinapenda sana kutoka sare?

oladipo

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2022
Posts
1,885
Reaction score
3,305
Wasalaam wakuu, hili suala nimeshaliona na kulifuatilia kwa muda mrefu sana. Nilichogundua ni kwamba hizi timu ndogo za ligi kuu bara huwa zinacheza kwa kutegeana ili zitoke droo na ikitokea timu moja imepata goli basi timu pinzani itapigana kutafuta goli la kusawazisha na wakifanikiwa kulipata wanapoozesha mchezo ilimradi lengo la kupata droo litimie.

Kwa walioangalia game ilioisha ya singida na kmc utaona kabisa timu zote zilikuwa zinapoozesha mchezo mixer kupoteza muda yaani wanakuwa wanaridhika na droo na hili lipo kwa timu nyingine ndogo za ligi kuu bara

Unadhani tatizo ni nini mpaka hizi timu ndogo zimekuwa ziki prefer kutoka droo kuliko kushinda?

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Mentality imejengeka vichwani mwao kuwa ushindi ni wa Simba, Yanga na Azam,

Wao wakipata sare, wakijiona wapo kwenye safe position (hawapo kwenye hatari ya kushuka daraja) bas ni full kurelax hata wafungwe sawa tu
 
Nyingi hupangwa mkuu

Nig kunamtutelegram toka asbh kaandkka FT X

Mechi ya singida na wametoa 0-0
 
Mentality imejengeka vichwani mwao kuwa ushindi ni wa Simba, Yanga na Azam,

Wao wakipata sare, wakijiona wapo kwenye safe position (hawapo kwenye hatari ya kushuka daraja) bas ni full kurelax hata wafungwe sawa tu
Duh! Yaani mechi zao zipo very predictable. Wanacheza kwa kutegeana.

Kiukweli hii sio afya kwa mpira wetu, watu wanalipa viingilio na kulipia ving'amuzi halafu wanacheza kwa kubembelezana ili watoke droo hii sio poa

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Ni ngumu kusikia labda Wamefungana 4-2, au 3-0 nk, ni mwendo wa 1-0 , 2-1 , 0-0 kwisha
 
Back
Top Bottom