Ukiangalia vita kati ya waisraeli na wapelestina utagundua moja ya silaha wanazotumia ni historia. Hapa kila pande inajitahidi kuonyesha kuwa kihistoria wao ndio wanastahili kumiliki ardhi wanayopigania. Hii inafanya historia kuwa ni moja ya silaha muhimu sana nchi inatakiwa kuwa nayo.
Mimi ni mmoja wa watu wenye shahada, Lakini mpaka leo huwa najiuliza nini kilichangia mpaka serikali ya Tanzania kuhamua kutumia kingereza kwa masomo yote sekondari ukiondoa kishwahili. Kwenye masomo kama fizikia na kemia naweza sema lugha yetu ni changa lakini kwenye masomo muhimu kwa maisha yetu ya kila siku kama histroria na uraia mpaka leo nashidwa kuelewa nchi ilikuwa inafikiria nini.
Maana nahisi kwenye kufundisha unahitaji mambo matatu muhimu:
Nilikuwa nikipenda sana somo la historia shuleni maana tulikuwa na Mwalimu aliyekuwa akijua kutusimulia vizuri (kwa kutumia kiswahili) jinsi mambo yalivyokuwa hapo nyuma. Nilipenda sana kumsikiliza lakini lilipokuja swala la kujibu mitihani hapa ndipo chuki yangu na hili somo ilianza. Sio kwamba sikujua nini cha kujibu bali lugha ilikuwa changamoto sana.
Kwa waliosoma software programming naamini wanajua kuna aina hizi 2 za testing:
Tukija kwenye maisha nahisi wengi tunaona jinsi vitu vingi tulivyosoma shule havina msaada kabisa. Hii tufanye ndio intergration testing.
Kuna muda nafikiria kuwa moja ya lengo kuu ya elimu ya Tanzania ni kututolea ujinga wa aina moja na kutuwekea ujinga wa aina nyingine. Kwa hili serikali inastahili pongezi.
Huwa nafurahi sana kusikia nchi nyingine zikianza kufundishwa kiswahili. Lakini sisi waanzilishi bado hatutumii kiswahili ipasavyo! Sijui nchi nyingine zitajifunza nini hapa.

- Urahisi wa kufikisha ujumbe kwa mwanafunzi wako.
- Urahisi wa kueleweka kwa mwanafunzi wako.
- Namna ya kupima uelewa wa mwanafunzi wako.
Nilikuwa nikipenda sana somo la historia shuleni maana tulikuwa na Mwalimu aliyekuwa akijua kutusimulia vizuri (kwa kutumia kiswahili) jinsi mambo yalivyokuwa hapo nyuma. Nilipenda sana kumsikiliza lakini lilipokuja swala la kujibu mitihani hapa ndipo chuki yangu na hili somo ilianza. Sio kwamba sikujua nini cha kujibu bali lugha ilikuwa changamoto sana.
Kwa waliosoma software programming naamini wanajua kuna aina hizi 2 za testing:
- Unit testing (Kupima kitu kimoja pekee)
- Intergration testing (Kupima kitu zaidi ya kimoja kwa pamoja)