Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 16,464
- 35,629
Wakuu ! Ni matumaini yangu mko salama na mnaendelea vyema na majukumu yenu ya kila kwa neema na kudra za Allah.
Nimeamua kuanzisha huu uzi ili niweze kusikia maoni yenu au kuweza kupata kujua ni namna gani ninaweza kupata haki yangu ya msingi hasa kwenye kipindi hiki ambapo upatikanaji wa haki kwa Mtanzania wa kawaida umekua ni mgumu.
Kusema kweli inaumiza sana moyo, akili na fikra pale ambapo mtu unakuwa umedhurumiwa haki zako na hata pale unapokuwa unafuata taratibu zote za kupata haki yako imekuwa ni mtihani mgumu sana.
Na hapa ndipo ninapoukumbuka wimbo wa Ney wa mitego Nitasema japo ulifungukiwa na kukatazwa na serikali kupitia BASATA usichezwa hadharani.
Ni hivi nilishawahi kuandika humu kuhusu kutumika kwa vyeti vyangu vya elimu na mtu mwingine. Nikapewa ushauri na watu humu niende baraza la mitihani (NECTA) Kukaguwa vyeti , lakini nikifukuzwa kama mbwa na yule mkaguzi wa vyeti vyangu na nililia kilio cha uchungu sana pale NECTA na yakatokea mambo mengine lakini nilikuwa tayari kwa lolote.
Bahati nzuri nilipata msaada kwa mdau humu humu jamiiforums nikaweza kumtumia softcopy ya vyeti alivyovihitaji na kweli yule mtu akaoneka yupo kwenye mfumo wa Wafanyakazi wa Serikali na alianza kufanya kazi kabla hata Serikali haijahamia Dodoma.
Mdau anasaidia virtually na hataki ijulikane public hili jambo na ninamshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa msaada wa huyu Mdau.
Kinachonifanya niandike huu uzi ni kwamba. Kuna Classmates wenzangu ambao tayari wapo kwenye mifumo tena ya ulinzi na usalama na wengine wamekula teuzi za Mkuu wa nchi, kila nikiomba msaada wa kuweza kupenya zaidi niweze kufanikiwa nao wamekuwa wakiniambia maneno ya kuvunja moyo na kutia hasira sana.
Maneno ya Classmates ni kama yafuatavyo.
1. Classmate no 1 ni RC wa Mkoa X nilipomwambia akaniambia anampa kazi PS wake na huyo PS wake hata simu yangu hapokei japo alipewa namba yangu na akanipigia tukabadirishana na namba.
2. Classmate namba 2 ni Afisa wa taasisi fulani nyeti naye nilimpigia akaniambia atanisaidia lakini cha kushangaza alinipa namba ya Mkaguzi wa vyeti ambaye alinufukuza pale NECTA na bahati nzuri huyo Mkaguzi wa vyeti sikuwa hata na namba zake za simu nimezipata zote mbili TTCL na VODA na huwa ninatumia true caller zimeniletea mpaka majina yake na nilivyo yaangalia kupitia kutuma Pesa yakaja vile vile, yule Mzee nilimfuata mweneo ya Corner Bar Sinza nikaongea naye na Nikamwambia nilishawahi kwenda NECTA nikafukuzwa hata vyeti havikuangaliwa kwenye system, akaniuliza na nani ?
Nikamwambia kuna Mzee alinifukuza na sumkumbuki vizuri (Kumbe ni Yeye) Mzee ana kiburi na majivuno sana ila nashukuru namba zake ninazo huko mbele za safari atajaa kwenye mikono wa sheria. Cha kushangaza hiyo siku ilikuwa Jumamosi baada ya kuongea naye na kumwachia softcopies za vyeti vyangu akasema atalifanyia kazi jumatatu akiingia kazini lakini baadaye anampigia simu yule X Classmate wangu kumwambia jina langu halipo kwenye mfumo wa malipo ya serikali na yule X Classmate wangu nikamwambia ukweli siwezi kukurupuka kufanya kitu pasipo na uhakika asante kwa msaada wako na huyo mtu uliyeniunganisha naye ndiye aliyenikatalia na kunifukuza kama Mbwa ile siku naenda kukagua vyeti vyangu pale NECTA.
3. X Classmate wa tatu ni Ofisa wa ngazi ya juu sana kwenye vyombo vya Ulinzi na Usalama naye nilimwambia ishu yangu akanishauri niende Polisi kutoa taarifa na wakati aliyenifanyia huu uhuni ni Afisa wa Polisi Mkubwa sana na madaraka makubwa sana kwenye usimamizi na uangalizi wa usalama wa Viongozi waandamizi wa Serikali. Huyu nikaamua kumsikiliza na kumuacha kama alivyo.
Nikaamua tena kurudi humu jamiiforums ndio nikapata msaada na mdau kajitolea ( Mkuu samahani kama utakuwa unanisoma lakini nawasilisha hisia zangu za machungu kwa wadau humu mtandaoni).
Najiuliza mpaka sipati majibu hivi ni
1. Kwanini Wafanyakazi wa Serikali wenye kutatua kero za Wananchi wamekua na viburi, dharau na majivuno kwa Watanzania wenzao wenye kutafuta haki zao za msingi ?
2.Kwanini Wafanyakazi wa taasisi za umma wamekuwa wakifanya mambo kwa ubinafsi na kujisikia pasipo kuuvaa ule mguso wa mtu mwenye uhitaji?
3. Kuna Ulazima wa kufanya tukio litakaloiacha mdomo wazi nchi nzima mpaka viongozi wa juu?
Nimeandika kuelezea hisia zangu tu lakini inaumiza sana akili, hisia hata roho. Ni nini kifanyike ili kuondoa hii dhuruma, uonevu na ukatili?
Nawasilisha.