Hivi kwanini wazee walitufanyia hivi?

Super Sub Steve

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2011
Posts
17,404
Reaction score
10,900
Yaani enzi za utotoni mambo yalikuwa ni shida sijui ndiyo vyuma vilikaza au sijui nini?
1.Nyama ilikuwa bei rahisi tu lakini Kula mpaka Sikukuu tena mnapewa kipande kimoja tu na mchuzi wa kutosha.Siku hizi maisha yamekaba nyama bei ghali lakini watoto wanakula nyama mpaka Meno yanauma.
2.Wali ndiyo ilikuwa anasa mpaka Sikukuu na ukipikwa siku hiyo Nyumbani unarudi mapema.

3.Kama hujafanya kazi za home siku hiyo Basi unanyimwa tu nyama hiyo ni bonge la adhabu.Unaweza ambiwa tu kwanini hujachota maji Leo huli nyama.Unakuta mtu unaanza kwenda kisimani saa mbili au Tatu usiku ili upate nyama.

4.Kwetu ilikuwa ukila Chakula cha mama aliyetoka kujifungua Basi utapata matundu (Ugonjwa ambao unatokana na Kula Chakula cha mama aliyetoka tu kujifungua au kushea Vyombo anavyotumia.
Hii ilikuwa ni uongo tu.Nilinyimwa nyama na Mzee,kisa sijachota maji bahati nzuri kukawa na nyama ya mama ambayo tulikuwa haturuhusiwi Kula.Nikafanya yangu nikala ile nyama sikuugua hata kidogo Wala sikuota vidonda (Matundu) kama ilivyokuwa inaaminika.Nikajua huu ulikuwa ni uongo tu.

Waliopitia haya na mengine mpo.Hivi kwanini wazee walitufanyia haya lakini.Ndiyo mana hata tabia za udokozi zilikuwa nyingi.Assume umekosa nyama home au nyama imetokea mara moja tu utachaje kudokoa?
 
Dah.....wazee wetu waliijua miiko mingi sana...tatizo tu hawakuweza kuelezea kisayansi...Kwa ufupi gramu 40 ( kama nusu mshikaki) unamtosha binadamu MTU mzima kwa wiki moja ....zaidi ya hapo unatia sumu mwilini....au kilo 1 ya nyama kwa watu 25 kwa wiki...au familia ya watu 4 inahitaji bajeti ya kilo 8½ tu kwa mwaka....kwasababu za kiafya..[emoji13]
 
Unaruhusiwa kumpeleka mahakamani, kwani alishindwa kukupa haki zako za msingi na alikunyanyasa sana


Make haya ndio vijana wa siku hizi mnayopambania
 
Ukute unadokoa kuku yaan wakati wa kupakua wanashangaa huyu kuku mbona ana mguu mmoja haa haaa utoto hatari sana
 
Dah... Kwahiyo ilimaananisha nini?
Nilimaanisha kuwa kwa maisha hayo aliyoeleza mleta mada ni unyanyasaji fulani hivi na maisha ya shida shida. Kama kula wali tu ilikua kitu cha anasa sasa ndio nikaona kwa sisi ambao tulikua hatuna limits zozote basi maisha yetu yalikuwa ni bata.. Changanua mambo.
 
Dah....bado hata sikusomiii[emoji13]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…