Hivi kwanini Yanga hawavai nembo ya mdhamini wa NBC PL?

Vyamavingi

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2014
Posts
5,818
Reaction score
5,555
Wadau wa soka naamini mko salama. Mimi nimeshaachana na ushabiki wa soka krk nchi yetu kwa sababu kadhaa ingawa huwa naifuatilia.

Juzi kumeibuka mvutano kati ya timu ya Simba na TFF kuhusiana na mdhamini mwenza GSM ambao TFF waliusaini bila kushirikisha wadau wengine wa NBC Premier League na wala hawakutaka wadau wengine wa ligi wauhoji; what a shame!

Uzi wangu unahusiana na ubabe wa Yanga kutovaa nembo ya mdhamini wa ligi kuu yaani NBC Premier League kwa kuwa nembo ya NBC ina rangi nyekundu! Huu ni ushamba na ubwege! Msimu uliopita wakati ligi kuu ikidhaminiwa na Vodacom, Yanga waligoma kuvaa nembo ya Vodacom kwa sababu tu ina rangi nyekundu na nyeupe kwa kizingizio kuwa katiba yao haitambui rangi nyingine zaidi ya kijani, njano na nyeusi!

Ikumbukwe kuwa nembo ni alama muhimu inayotambulisha kampuni husika na ndio maana huwa zinasajiliwa kwa sheria za kitaifa na kimataifa na kwa jinsi hiyo hakuna kampuni wala mtu anayeweza kutumia nembo iliyosajiliwa bila idhini ya mwenye nembo.

Rangi ni muhimu sana kwenye nembo yoyote na ndio maana hakuna nembo isiyo na rangi. Nembo insposajiliwa kama trademark pamoja na alama nyingine rangi zake pia huhesabiwa kuwa ni sehemu ya nembo. Ndio maana huwezi kukuta Cocacola ina rangi zaidi ya nyekundu, nyeupe au nyeusi. Ukikuta soda ya cocacola imewekwa kwenye kadha au chupa iliyoandikwa cocacola kwa rangi ya bluu na kijani huwezi kuthubutu kuinunua kama cocacola.

Kwa maana hiyo, Yanga, kwa misimu miwili sasa imekuwa ikiingia kwenye mivutano na TFF na wadhamini wa ligi kuu kwa kugomea kuvaa jezi zenye nembo za wadhamini. Huenda hata kujiondoa kwa Vodacom kwenye udhamini wa ligi kuu kumechangiwa na upuuzi huu maana hakuna nembo ya Vodacom yenye rangi nyeusi! Vivyo hivyo, nembo ya NBC haina rangi nyeusi, ile sio nembo ya NBC inayofahamika, kutumia nembo ya NBC ikiwa rangi tofauti na zilizosajiliwa kisheria ni kosa kisheria kwa kuwa nembo rasmi ya NBC haina rangi nyeusi.

Ifike wakati TFF na Wizara husika wakae na vilabu vyote vya ligi kuu na waje na suluhisho la suala hili, ikiwa kila klabu itadai kutotambua nembo ya wadhamini wa ligi kwa wakati husika itakuwaje? Kila klabu ikitaka nembo ya mdhamini ilingane na rangi zao timu zao itakuwaje? Tiache kulea ujinga, mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. Kama klabu haitaki kutambua nembo ya mdhamini basi isipewe haki ya kupokea chochote kutoka kwa wadhamini.

BTW, nikija kwenye suala la Yanga kugomea rangi za nembo ya mdhamini mbona walishiriki michiano ya CAF champions league na walivaa nembo ya Total ambayo ina rangi nyekundu? NAWASILISHA.

Vv
 
Mkuu naomba nikusahihishe.... Yanga hawakuvaa nembo ya TOTAL..... ile inavaliwa kuanzia hatua ya makundi kama sikosei.... Wao waliishia play off.
 
Thibitisha hapa kwa picha kuwa Yanga havai N BC
 
Mkuu naomba nikusahihishe.... Yanga hawakuvaa nembo ya TOTAL..... ile inavaliwa kuanzia hatua ya makundi kama sikosei.... Wao waliishia play off.
Kwa hiyo ni kusema wangekataa kuivaa kama wangefika makundi ya CAF champions league?

Vv
 
Haya ndio madhara ya kunywa gongo ikiyochacha mtakuja kutufia bure...

Hivi kweli uliona hawavai logo ya mdhamini mkuu? Kweli?
 
hawajui hata nembo ya Total inafananaje hiyo huvaliwa na wajanja waliozoea kuingia hatua za makundi huko CAf hawa level zao ni mapinduzi cup
 
Kwa hiyo ni kusema wangekataa kuivaa kama wangefika makundi ya CAF champions league?

Vv
Hapana mkuu. Hawana uwezo huo... Hata wangeambiwa wavae jezi nyekundu wangevaa. Tatizo ni hawakuwa na uwezo wa kufikia hadhi ya kuvaa hiyo nembo.
 
Haya ndio madhara ya kunywa gongo ikiyochacha mtakuja kutufia bure...

Hivi kweli uliona hawavai logo ya mdhamini mkuu? Kweli?
Unajua maana ya logo? Umewahi kuona logo ya Cocacola ina rangi ya njano?

Vv
 
Wewe ambaye unabisha ndio uthibitishe kwa picha kuwa wanavaa.

Vv
Nathibitisha
IMG_20211213_165617.jpg
IMG_20211213_165545.jpg
ukiangalia hapo kwenye bega unaona nembo ya NBC
 
Unajua maana ya logo? Umewahi kuona logo ya Cocacola ina rangi ya njano?

Vv
Mkuu kifupi Yanga ni dude fulani hivi kubwa kubwa,Yaani ukubwa wake hauelezeki.

Linapokuja suala la Yanga akitaka jambo lake basi hakuna wa kumzuia si TFF wala TPLB.

Kwa kulijua hilo ndio maana Yanga wanafanya wanavyotaka na hakuna mtu wa kupinga.

Walibadili rangi ya logo ya Vodacom na sasa amebadili rangi ya logo ya NBC.
 
Kiufupi wewe ni mpumbavu baki na ujinga wako, maana hata ukielezewa utakaza mshipa wa tako tu.
Dogo punguza jazba, nimetoa elimu kuhusu logo na trade mark lakini huelewi. Hebu tembelea Copy Right Act uone kama hoja zako zina mashiko.

Basi mkuu, Yanga hawavai logo ya NBC kulingana na hoja yako. Haya nenda kawasaidie NBC bank kuishati yanga kwa kutofuata mambo ys copy right Act.
 
Mkuu kifupi Yanga ni dude fulani hivi kubwa kubwa,Yaani ukubwa wake hauelezeki.

Linapokuja suala la Yanga akitaka jambo lake basi hakuna wa kumzuia si TFF wala TPLB.

Kwa kulijua hilo ndio maana Yanga wanafanya wanavyotaka na hakuna mtu wa kupinga.

Walibadili rangi ya logo ya Vodacom na sasa amebadili rangi ya logo ya NBC.
Yanga Ni kubwa kwa Ihefu Ila kwa River Wana manuka nje ndani.
Alafu ili kuthibitisha kuwa nyie Ni wakubwa fikeni makundi club bingwa alafu mkagome kuvaa TOTAL hapo ndio mtakua wakubwa .

Yanga Ni sawa na mjanja wa Kambasegera akifika Bongo Daslam anakua boya tu.
 
Dogo punguza jazba, nimetoa elimu kuhusu logo na trade mark lakini huelewi. Hebu tembelea Copy Right Act uone kama hoja zako zina mashiko.

Vv
Hueleweki
Ulianza kusema hawavai tumekuonesha picha.
Saizi umekimbilia kwenye rangi sijui trademark yaani unataka ubishani tu.

Wamevaa au hawajavaa?
Halafu mimi sio dogo sawa janja?
 
Yanga Ni kubwa kwa Ihefu Ila kwa River Wana manuka nje ndani.
Alafu ili kuthibitisha kuwa nyie Ni wakubwa fikeni makundi club bingwa alafu mkagome kuvaa TOTAL hapo ndio mtakua wakubwa .

Yanga Ni sawa na mjanja wa Kambasegera akifika Bongo Daslam anakua boya tu.
Simba nayo ni kubwa kwa JKT ila kwa Galaxy anapigwa thalatha tena hapa hapa kwa Mkapa![emoji16][emoji16]
 
Back
Top Bottom