Hivi kwanini Zanzibar tusiipe ban hata ya mwaka 1 tu kwenye muungano ili wawe na adabu?

Hivi kwanini Zanzibar tusiipe ban hata ya mwaka 1 tu kwenye muungano ili wawe na adabu?

mwekundu

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2013
Posts
21,859
Reaction score
19,736
Naomba kuwakilisha ni mtazamo wangu tu kimaono,nimefikia hatua hiyo kutokana na harakati za wanzanzibar mbalimbali mara tu tangia huu muungànò mwaka 1964 kulalamika kuwa wanaonewa na kuanza kuunda makundi mbalimbali kuupinga na hata muda mwingine kusababisha maafa na hasara mbalimbali
Hivi karibuni kuna kikundi amabacho kinaitwa UAMUSHO,ni mamlaka ambayo ukichunguza kiundani iliundwa kwa misingi ya kidini-ifanye harakati za dini Zanzibar,chakushangaza ajenda yao kuu ni kudai muungano uvunjwe wanadai sio wa haki wanataka zanzibar iwe nchi huru!
Hawa watu kadiri siku zinavozidi kwenda wana gain political interest kubwa zanzibar kwa mgongo wa dini kitu ambacho ukiwa mchunguzi wa kina ni hatari kinaweza hata sababisha kutangazwa JIHAD wakiendelea kukandamizwa kama inavofanyika sasa hivi
Serikali yetu kwa busara zake za kuuenzi muungano wamejikuta wakitumia nguvu nyingi kutuliza hivi vikundi kitu ambacho si kizuri kwani kadili inavozidi kuwakandamiza wanawatia usugu wakuendeleza mapambano yao dhidi ya Zanzibar nchi huru
Napenda kutoa angalizo langu binafsi la mwandishi wa thread hii kuwa ipo siku wataibuka MA SUICIDE BOMBER ili mradi tu wahakikishe malengo yao yanatimia
Watapandikiza watu wajiripue mabomu hapa kwa pazia la JIHAD wakati kiundani zaidi ni sababu za kisiasa(political interest) na jinsi watanzania tulivo wasahaulifu tutasahau kwamba hawa jamaa tangia enzi za Karume na Nyerere walikuwa wanadai utaifa wao na tutawapiga au kuwasemea kwa propaganda ya udini suala ambalo itakuwa rahisi tu kwa wakristo na waislamu wa Tanzania bara kuamini kuwa ni kweli udini na vita hii kusambaa (kuambukizwa) huku bara tuliko
Ni lazima ikumbukwe kuwa hawa watu wamedai sana terms za muungano kuangaliwa upya au kuvunjwa tangia enzi za 1964 hadi hatua ya MAHAKAMA na juhudi zao kukwamishwa makusudi bila kupewa maJibu yanayoeleweka hii yote kwasababu ya ukweli uliomo ndani
Nahitimisha kwamba wanachogombea wanzanzibar kunakiukweli fulani lakini kiuhalisia hawawezi kujitawala kwasababu ya ubaguzi wa PANDE mbili wao kwao(huu ni aina ya ubaguzi ambao ni mbaya sana unahistoria ya vita na mauaji ya genicide_kimbali) ,Hii sio kwa sababu tu watu wa bara tuliwadumaza tangia mapinduzi ya Zanzibar bali pia ni historia ya uhasama wao wa asili wa UUNGUJA na UPEMBA. Ndo mana late Mwl Nyerere alisema kuwa dhambi ya ubaguzi itaendelea kuwatafuna hata kama wakijitenga na bara,ndo mana Karume aliona mbali na kujali utaifa mbele bila hata kuangalia terms vizuri za muungano akauunga tu ili kulinusuru hili janga wanalolidai wao kwa nguvu zote
Mimi wazo langu wamelia saana vya kutosha tuwape tu ban au muda tuwape hata mwaka mmoja nina hakika lazima watarudi wanamajeraha na kuudai kwa nguvu muungano
Ukitaka kuhakikisha hili utaona tu viongozi wa Zanzibar baadhi yao wanahitaji muda mwingine hawahitaji(unafiki) wanajua madhara yake,Hta maalifu Seif ni mnafiki namba moja kwani ajenda ambayo anafahamika kwa mvuto wa kisiasa Zanzibar ni kuuvunja Muungano cha kushangaza alikubali mwaka 2010 kutumikia serikali hiyohiyo na sasa anaona muda wa uchaguzi 2015 unakaribia anaanza kutoa kauli za ajabu ajabu ili azivune kura za wananchi

WSent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
FACT:
Hawabebeki....Na viongozi wao ni DOUBLE STANDARD urojo mtupu !!
 
Ni kweli wanaonyesha hawana msimamo mfano maalim Seif ni two in one


Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
Vijana wa zanzibar wakijitokeza patakuwepo na mabadiliko lukuki, La ajabu Viongozi wazee ni mzigo kwa maendeleo....
Yaani hao kwa hao viongozi hawana ubunifu wakujikimu, Sera zao vuguvugu kisingiizo na kulalama, hawana jipya, Vijana wapo lakini wamenyimwa haki. Sasa itakuwaje hakuna zuri la kutegemea .... Poleni wandugu
 
Sio kweli kuwa watanganyika wanataka muungano wao wanataka kuendelea kuitawala zanzibar kiujanja ujanja na hilo sasa basi. sisi tunajiweza kwa nini mutubebe huu sio wakati wakubebana kila mtu atajua vipi atafika anapokusudia kufika.

Tatizo sio zanzibar kudai mamlaka kamili tatizo ni Tanganyika kutokujiamini kuwa na wao wakitaka kuwa nchi kamili wanaweza. kwani watu wakiwa ndugu lazima waendelee kuishi nyumba moja? tumechoka kubebwa wacheni tutembee kwa miguu yetu speed yenu ndogo sana katika kuleta maendeleo yetu.

Ndugu muandishi nasikitika sana kuwa wewe sio mkweli katika hoja yako eti wazanzibari hawatoweza kujitawala na ukajifanya umesahau kuwa katika Africa mashariki na kati hakuna dola kongwe kuliko dola ya Zanzibar na hii ilijumuisha mwambao wa waafrica mashariki kuanzia msumbiji hadi south somali hii yote ilikuwa ni dola ya zanzibar ikiwemo tanganyika vipi leo unathubutu kusema eti sisi hatuwezi kujitawala isijekuwa tatizo hilo liko tanganyika kwenye history ya vita va makabila.

kwa ufupi hakuna records zinazoonyesha watu wa pemba na watu waunguja ni maadui waokwa wao na pia hakuna history ya vita vya wenyewe kwa wenyewe zanzibar. kwa hiyo sisi tunajiamini tunaweza kuishi ndani ya muungano na pia nje ya muungano na kama nyinyi tanganyika mnaweza challenge ipo mbele yetu fanyeni kweli tuone kwa kumalizia niseme " wazanzibari ni walimu wa siasa na kwa siasa kabisa tutaipata zanzibar yenye mamlaka kamili"
 
Mbona watanganyika mumeng'ang'ania kwamba Z'bar nje ya muungano kuna Unguja na Pemba basi kwa taarifa yenu jambo hilo kwa Z'bar kamwe haliwez kutokea kwa sababu hakuna tofauti ambazo zina weza kuibuka na kuligana taifa la Z'bar ukilinganisha na Tanganyika kuna tofauti kubwa ya kidini,na kikabila kwa wana nchi wake
 
Kabla ya muungano Zanzibar ilikuwepo, ndani ya muungano Zanzibar ipo, nnje ya muungano Zanzibar itakuwepo, simple and pure.
 
Back
Top Bottom