Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Au huenda hawajabadilika ulikuwa huwajui vizuri!
Miaka takribani arubatashara iliyopita tukakutana pale uwanja wa ndege wa kimataifa wa Ivato, jijini Antananarivo kisiwani Malagasi.
Wote bado tulikuwa washababi na watanashati wenye nyuso zilizojaa furaha na bashasha.
Wewe hukuwa na shaka na ufarashi wangu nami vivyo hivyo sikuwa na shaka na wa kwako.
Tumepitia mengi, njia tambarare, milima, pamoja na mabonde.
Nini kilichokusibu ghafla umebadilika? Wewe hutaki kuambiwa. Hutaki kusemwa.
Unashawishika na mambo madogo. Unashawishika na vitu vidogo.
Hivi kwa nini? Kwa nini watu hubadilika na kuwa kama siyo wao tena?
kwenye bold maana yake nini?
By the way, malagasy ni lugha nchi ni madagasikara
Sasa lipi ni lipi? Ni kwamba watu hubadilika tabia zao au mlipokutana walificha tu rangi zao?
Mtu utajuaje kuwa lipi ni lipi?
Dah huwa inauma sana,ila sababu kuu ni kuwa wanakua wamechoka......wanahitaji changamoto mpya!
changamoto hizo ndo zinazoumiza mioyo yetu...wakati tunashangaa imekuaje,wao hata hawajali...
If you feel that God is so far away, guess who moved?
My favourite quote.
Relevance yake hapa ni kuwa, huenda wewe ndo umebadilika. NN, signature yangu unaweza kuitafsiri vipi kwenye ulimwengu wa mahusiano?
If you feel that God is so far away, guess who moved?
My favourite quote.
Relevance yake hapa ni kuwa, huenda wewe ndo umebadilika. NN, signature yangu unaweza kuitafsiri vipi kwenye ulimwengu wa mahusiano?
Binadamu habadiliki, ila huficha makucha yake mwanzoni.
Watu tunapenda tujulikane kwa mazuri yetu na si mapungufu yetu.
Tukiwa wapya, naficha yote mabaya hadi nikuzowee.
Arubatashara=14
Shababi=kijana, vijana, ujana
Malagasy is an adjective referring to Madagascar. It may refer to:
- Malagasy people
- Malagasy language
- Malagasy culture
- Malagasy Republic
- Something related to the island of Madagascar
Nilikuwa madagascar 1999, na hiyo ni 13 yrs ago .......
Nilifikiri ulitaka kuita jinsi wao wanavyoita nchi yao ndio maana nikakukosoa, by the way it would ave felt better kama ningekunail hata once. LOL
Ukishanizoea unaficha mazuri. Kongosho bana! Khaa!
ha ha ha ha, yaani wee mkorofi sana.
Haya tu, hili dongo nimelipokea kwa mikono miwili.
Huwezi kuuita utapeli manake mmekaa miaka mingi sana ingekua muda mfupi sawa...ni ukichaa tu..wa kujaribu vitu vipya lakini baadae huwa unaisha,..ghafla kama ulivyoanzaJe, ni sawa tukiyaita hayo mabadiliko kuwa ni utapeli wa kimapenzi?
Nadhani umetumia handheld device kubandika hili bandiko kwa sababu halina hiyo signature yako.
Yap yap, nokia tochii bana!
Au visa vya maxence manake nae hajachacha!
Lets give another try...