Hivi kweli Burundi inatoa wataalamu wa soka kuishinda Tanzania?

wazunguwawili

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2019
Posts
3,984
Reaction score
4,132
Kwa siku za karibuni tumeshuhudia Burundi ikileta watu wake kupata ajira hapa Tanzania.

Kuna makocha,tena wapo timu kubwa kabisa.

Achilia mbali lundo la wachezaji waliopo katika vilabu vyetu.

TFF isifanye nchi yetu shamba la bibi,ndiyo maana soka haliendi mbele.
 
Mkuu usistaajabu, Sasa kama viwanja vingi vya wazi na michezo vimeshauzwa au kuwekwa miradi ya kuingizia mapato halmashauri na manispaa ili kufika malengo la kukusanya mapato unategemea nini? Hivyo vipaji na wachezaji mnapata wapi?
 
Burundi kiuhalisia ni sehemu ya Tanganyika. Kimipaka ndio inaitwa Burundi, hapo awali ilikuwa ilifahamika Ruanda-Urundi iliyokuwa imeshikana na Kagera na Kigoma baada ya mipaka ikitokea (Rwanda na Burundi).

Katika Soka, huwezi kulalama kama huna uwezo. Nchini Uingereza asilimia 65 ni wachezaji na wakufunzi kutokea mataifa ya nje.
 
Usiumize kichwa sema dunia nzima ilikuwa sehemu moja. Wapuuzi wachache ndio wakaweka mipaka wa huku wa huku wa kule wa kule
 
Mkuu ulicho sema ni kweli lakini niseme kitu kimoja nakumbuka miaka ka 10 hivi nyuma niliwahi kuona progrem yakukuza vipaji na marehe Rais wao aliisimamia kwa nguvu zake zote tokea awamu yake ya kwanza, na tuliwahi kusema pale Buja hawa jamaa baada ya miaka 10 mbele watakuwa hatari kwetu na kweli imekuwa.

uzembe,ulafi, nakutokuwa waaminifu ndicho kinacho tuponza. Nina mfano wa ofisi ya TFF ya kwetu tulipewa pesa sawa sawa na Zambia wakati inaongozwa na Kalusha Bwalya laikini yule jamaa alitushinda akajenga ofisi ya maana kuliko sisi, hata wale jamaa wa maendeleo ya soka walipo kuja walitushangaa sana. Aliye turoga sijui alitumia njia gani.
 
Mkuu tuangalie kwao wamefanikiwa nini?

Ukiona hata wana mipango bora kuliko sisi basi hicho tu kinatosha.
 
Kauli yako ni kama unaidharau Burundi

Unataka kusema wao hawatakiwi Kutushinda?

Binafsi jicho langu linaona ligi yetu imekua kivutio na ina tija zaidi ya nchi zinazotuzunguka

Ndio maana kila mtu anataka kucheza au kufundisha mpira Tanzania.
 
Kwanza Burundi wangekuwa na rasilimali tulizonazo wangekuwa mbali si unaona ka Rwanda kanavyotutoa jasho
 
Kuna interview moja ya Ndayiragije na Clouds fm alipokuwa ndo kakabidhiwa Starz, alisema kwamba alipokuwa anasoma kozi ya ukocha ili kupata leseni daraja A ya UEFA nchini Germany alikuwa na wenzie wa Burundi kama 10 hv ambao aligraduate nao, lakn pía akasema kile chuo ndani ya miaka 3 walishapita raia wa Burundi takribani 100

Na akaongezea pía kuwa wengi wao wametapakaa nchi mbalimbali duniani kutafuta fursa za ukocha kwakuwa wengi wao wana leseni cha ukocha daraja A ya UEFA

Hvyo kwa namna hiyo unaweza kuona ni namna gani jirani zetu wamepush na wanapush sn ktk angle hio ilhali nchini kwetu watu kama kina Matola, Nizar Khalfan, Zubeir Katwila wapo timu kubwa afu vijana lakn hawana hata angalau leseni ya ukocha daraja B ya CAF

Wachache kama kina Hemed Morocco, Dennis Kitambi, Master Charles Boniface Mkwasa nk ndio angalau wamejiimarisha ktk vyeti
 
Kabla ya kuanza kulalamika jiulize kwanini mnashindwa kutoa marefa kwenye michuano ya Africa wakati timu zenu zinashiriki huku waburundi tunawaona wakichezesha mechi mbalimbali
 
Inaumiza na kukera kiasi napata kigugumizi kukiri ukweli kwamba, hata timu yetu ya taifa inaposimama na timu ya taifa ya Burundi basi huwa tunasimamishwa! Huo ndo ukweli wenyewe, hata kama ni mchungu, umezee kwa maji baridi!!



Kimoko hicho mzee baba, tena HOME!!
 
Kwakweli warundi niliwaona kwa macho yangu wanavyo andaa vituo na walikuwa wana mpango wa muda mrefu sio kidogo, na kampunu niliyokuwa nafanyia kazi wajkati huo tulikuwa tuna beba container za hiyo miradi sana maana walikuwa wanaagiza vifaa nnje ya nchi na hawakujenga hivyo vituo kimzaha waliwekeza kweli.
 
Matola ni kijana?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…