Hivi kweli kaskazini kuna katika katika umeme kuliko mikoa mingine kama Dar na Mwanza? Dalili ni kama tunapigwa live!

Hivi kweli kaskazini kuna katika katika umeme kuliko mikoa mingine kama Dar na Mwanza? Dalili ni kama tunapigwa live!

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2013
Posts
11,550
Reaction score
40,697
Rais ametoa tamko rasmi kuwa serikali imesaini (itasaini?) mkataba wa kununua umeme kutoka Ethiopia ili kuondoa kama sio kupunguza kabisa tatizo la umeme kukatika katika ovyo katika mikoa ya kaskazini.

Huenda labda sina taarifa sahihi, lakini sote tunajua kukatika katika ovyo kwa umeme kupo nchi nzima lakini kuna maeneo na mikoa fulani ambayo hukumbwa zaidi na hii kadhia hususani Dar na Mwanza ambapo huhitaji na matumizi ya umeme ni makubwa kupitiliza kiasi ambacho athari ya kukatika umeme huenekana haraka na kwa ukubwa sana.

Soma Pia: Rais Samia: Serikali itanunua Umeme nje maalum kwa Mikoa ya Kaskazini

Kuna kaharufu fulani kaupigaji kwa kutengeneza tatizo na kisha kukatafutia suluhisho la kimagumashi ili kupiga pesa.
 
Mulemule kaka, kila anayekuja anatafuta kupiga kwenye umeme. Maneno tu yanabadilika, huyu mitambo imechoka tununue. Hakuna anayejali wala kuhoji, wakishapiga pesa hata yakibumbuluka hakuna wa kuwajibishwa, maisha yanaendelea.
 
Usishangae umeme wa tanesco unapekwa nje then wanarudisha wahuni wapige pesa🤣🤣

Abdul rostam na ... Ogopa sana
 
Lile bwawa walisema mkandarasi anakabidhi soon imekuwaje tena.
 
Utapeli.

ZimePita zaidi ya week 3 umeme haujawahi kukatika kwa zaidi ya lisaa 1.

Kwa maana nyingine umeme unakatika kwa wastani kila baada ya siku 4 au zaidi na huchukui zaidi ya lisaa 1 unakua umesharudi.
 
Sometimes wananchi wasipobadilika tutapelekwa hivi hivi. Kwa sababu stori za kununua au kuuza umeme nje ya nchi sio za leo wala jana, ni miaka nenda Rudi. Na Cha kushangaza miaka mitano watarudi na stori hizihizi
 
mmh! mafisadi yashaweka mrija wa asali hapo..baada ya aggreko,IPTL na Songas kumaliza mikataba yao itakuwa mafisi yamekosa ulaji..maana kipindi hiko Tanesco ndio walibebeshwa zigo la kununua umeme na walikamuliwa sana kwa kuyalipa mabilioni ya hela makampuni ya umeme kina IPTL na wenzake Capacity charge za milioni 100 kila siku..ndiomaana ngosha akajenga bwawa la stigle gorgle kukata hii mirija ya wahuni mana unyonyaji ulizidi..tangu haya makampuni yamalize ile mikataba yao ya kinyonyaji Tanesco ikawa imepumua.. ila bado kuna mafisadi wamefanya tanesco ni kichaka cha ulaji bado wanataka kurudisha biashara za umeme na kama kawa zigo la malipo ya manunuzi ya huo umeme atalipa Tanesco na hapo mafisadi watapata cha juu huko mbele kwa kuchonga dili..
 
Mbinu za upigaji watu wanataka kuiacha nchi kwenye umaskini wa kutupwa huku wao wakiwa mabilionea
 
Rais ametoa tamko rasmi kuwa serikali imesaini (itasaini?) mkataba wa kununua umeme kutoka Ethiopia ili kuondoa kama sio kupunguza kabisa tatizo la umeme kukatika katika ovyo katika mikoa ya kaskazini.

Huenda labda sina taarifa sahihi, lakini sote tunajua kukatika katika ovyo kwa umeme kupo nchi nzima lakini kuna maeneo na mikoa fulani ambayo hukumbwa zaidi na hii kadhia hususani Dar na Mwanza ambapo huhitaji na matumizi ya umeme ni makubwa kupitiliza kiasi ambacho athari ya kukatika umeme huenekana haraka na kwa ukubwa sana.

Soma Pia: Rais Samia: Serikali itanunua Umeme nje maalum kwa Mikoa ya Kaskazini

Kuna kaharufu fulani kaupigaji kwa kutengeneza tatizo na kisha kukatafutia suluhisho la kimagumashi ili kupiga pesa.
Zinasakwa hela za kuhonga wananchi na kuwalipa vijana wa ccm kufanya ukatili, na vyombo vya dola kufanikisha ushindi wa dhuluma wa ccm.
 
Badala ya kununua Umeme huenda tungewakodisha wao waje watumie hivi vyanzo vyetu lukuki huenda tungeuza hata Afrika nzima....

Ila ukweli ni kwamba kinachokosekana ni uroho na huruma ya wananchi na mali za taifa..., hakuna kinachoshindikana lakini imekuwa miaka nenda rudi ni same Script Different Cast...

Tuache kucheza na Nishati ina impact kubwa sana kama ni Asali mbona kuna sehemu nyingi za kulamba ?; Badala ya kuhangaika na kugawa mitungi ya gesi na kuwafanyia biashara mataifa ya nje angalau wangerudisha hata tariff zero (After all si Uzalishaji umeogezeka)

Lakini ndio hivyo hili zimwi linalotujua linataka kututafuna na kutumaliza....

Alijisemea Nesta Marley In abundance of Water a Fool is Thirsty...
 
Thread Hizi Lumumba FC Buku Saba Huwaoni Maana Nao Wanaona Aibu
 
Mulemule kaka, kila anayekuja anatafuta kupiga kwenye umeme. Maneno tu yanabadilika, huyu mitambo imechoka tununue. Hakuna anayejali wala kuhoji, wakishapiga pesa hata yakibumbuluka hakuna wa kuwajibishwa, maisha yanaendelea.
Fedha za uchaguzi hizo. Nani atakaye hoji?
 
Sa100 et al ni muendelezo wa mafisadi tu kama wengine.
 
Utapeli.

ZimePita zaidi ya week 3 umeme haujawahi kukatika kwa zaidi ya lisaa 1.

Kwa maana nyingine umeme unakatika kwa wastani kila baada ya siku 4 au zaidi na huchukui zaidi ya lisaa 1 unakua umesharudi.
Wapi huko? Huku Arusha baadhi ya maeneo umeme umekuwa kama anasa, unakata kuanzia asubuhi unarudi usiku, wajasiriamali wadogo wadogo tunaotegemea umeme wa tanesco tunataabika sana tangu kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake
 
Back
Top Bottom