Hivi kweli mama zetu ndio wawe watunzaji wa mali zetu? Mnawajua mama zetu walivyo?

Bora jasho liliwe na mama yako kuliko mdangaji mmoja anaeamini mahusiano ni source ya income
100% acha azile zoteeee kwanza huwezi kulipa fadhila za mama hata umpe dunia yote hii, me ata akifuja mali zangu ni sawa tu. Mke ni special sana ila kwa mama hagusi hata nusu ya thamani yake
 
Hiyo sio maana ya next of kin. Next of kin ni mtu ambaye atakuwa wa kwanza kutafutwa endapo litatokea na kutokea na sio kwamba ukiandikwa next of kin ndo mrithi wa Mali.
 
Umechanganya nambo. Hakimi hakumfanya mama yake awe msimamizi au muendelezaji wa mali zake. Hakimi alimfanya mama yake kama ndio mmiliki wa mali kwabiyo ni kama mama alimwajiri Hakimi aziendeshe mali zake.

Ni kama bakresa ni mwenye mali lkn kwa sasa shighuli za uendeshaji mali amewaachia watoto wake.

Halafu mother ako inaonekana ni b..... au basi.
 
Acha upuuzi,
Kwani kumpa mama umiliki hilo si ni jina tu kwenye makaratasi. Habari za uduni hazitatokea kwakuwa mimi ndiye director wa kila hatua.

Yaani bado utoto wako unakuaminisha kuwa mke yuko upande wako?
 
O Oyaa kama wanawake wameshakuloga usifosi tufanane mama ndio kila kitu wewe muandikishe mkeo usituletee ujinga hapa wakujifanya nice guy
 
Kwa hiyo wale wamama wa kule kaskazini wanaovuka boda kwenda kupigwa miti kule Kenya ni watakatifu?

Ama wale mama wa kule Arusha wanatafuna mrungi na kutupia konyaji kama maji ndio wapambanaji?
Ndio, kama unabisha kunywa wewe konyagi na tumia mirungi ndio unatakapo jua kuwa wama wale ni vyuma kweli kweli.🤪
 
Sema "mama yako" siyo "mama zetu" usigeneralize... Kila mtu atashika msalaba wake mkuu kwenye maisha binadamu hatufanani, kilicho applicable kwa huyu kina weza kisiwe applicable kwako. Just deal with what life gave you.

Conclusion: We Are Not The Same. Thread Closed.
 
Stop this nonsense and unproven generalization. Hivi mama samia ni nani vile?
 
Bila shaka utakuwa mwanamke wewe.
 
Stop this nonsense and unproven generalization. Hivi mama samia ni nani vile?

Umefanya kitu kinaitwa strawman fallacy kitaalamu. Yaani unataka kuhamisha mada kwa swali lako

Pia Mama samia anatoka Zanzibar. Na pia hoja yangu imeongelea mambo ya kusimamia pesa hata kwa wanawake ambao hawajaenda shule. Kati ya wa bara na wa pwani

Mama samia mwenyewe analaumiwa kwa matumizi mabovu kwenye awamu yake. Mikopo mingii.. watu wanatumbua tu

UNAWEZA UKAWA RAIS ILA BADO UKASHINDWA KUSIMAMIA FEDHA VIZURI. WANANCHI WAKALALAMIKA
 
Kuna sababu zilizomfanya afanye hivi,huwezi jua maisha yake na mke wake yalikuaje hatuwezi jua,nafikiri kuna ya zaidi yanayomfanya afanye hivi, kwanza kitendo cha mwanadada kudai NUSU ya utajiri wa mume wake tayari linaleta alama ya kuuliza angesema tu anataka asilimia kadhaa.....sasa mfano mzuri kaka yangu aliumwa serious kidogo tu mke wake akaanza kusema niandikishe jina langu ile nyumba unayojenga sijui wapi niandikishe jina langu sasa imagine MTU anaumwa unamwambia maneno hayo unataraji nini? Haya kapona sasa unazan kutakua na imani tena hapo?
 
Sema Mama yako ndio ana hayo mapungufu,,,na usijumuishe Mama wa wengine!!!!
 
Hakuna Strawman fallacy in my statement. Wanawake wa bara wengi wako chini ya wanaume na mwanaume ndio muamuzi wa kila kitu kuanzia matumi ya fedha (pesa ambazo ni za mwanaume hata kama alitafuta mwanamke) hadi personal decisions ambazo logically alitakiwa kufanya mwanamke.
Kusema mwanamke wa bara ana elimu juu ya matumizi bora ya fedha ikiwa hana authority kwenye familia ni mfano hai na maana sahihi ya fallacy arguiment.
 
Naye pia ana watoto nao watamwandikisha Mama yao awe mmiliki kwahiyo yeye awasomeshe tu ila akili zao zitakuwa kwa Mama yao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kataa ndoa
Kataa ndoa
Kataa ndoa
Ndoa ni ujambazi
Kuna lijitu limesha toka kapa huko[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Eti nusu kwa nusu[emoji1787][emoji1787]

Kwanzia kesho naenda kwa mwanasheria wangu mavitu yooote mpaka mbwa na kuku naenda kuvihamishia kwa bibi[emoji1787][emoji1787][emoji1787] hapo ndio lugha tutaelewana

Jamaa katoa code muhimu sana
 
Kama humuamini mama yako kaa na mtizamo wako. Huwa wanasema huyu alikuwa mke wa fulani Ila hawajawahi sema kuwa huyu alikuwa mama/Mtoto wa fulani.
Yaani uhusiano wa mwanamke huwa unaisha.

Unachoongea unaona kilichompata eboue wa Togo akatolewa jasho lake na m belgiji ,ama unaongea tu. Pia una uhakika gani Kama mkeo anakupenda kwa dhati unajuaje labda anaishi na wewe kwa sababu iko ivyo Kuna kuolewa/kuoa.
Mwanamke sio ndugu yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…