Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Sote tunataka nchi yetu isonge mbele lakini tunachoka na kuumia mnoo tunapoona suala la umeme hapa Tanzania kwa zaidi ya miaka 30 mfululizo likitumika kama kichaka cha upigaji wa watu fulani fulani na kuchezewa sarakasi za ajabu na wanasiasa.
Kwa muda mrefu sababu za kukosekana kwa umeme wa uhakika kwa muda wote ilikuwa ni uhaba wa uzalishaji wa umeme. Na sababu za kukosekana umeme wa gharama nafuu zikawa ni zile zile za kukosekana vyanzo vya maji vya kutosha kuzalisha umeme huo.
Ujenzi wa Bwawa la Nyerere ukaonekana ndio suluhisho kamili, bwawa likajengwa kwa gharama kubwa sana na kuweza kuzalisha umeme wa kutosha mahitaji yetu yote ya sasa, mahitaji yanayotegemewa siku za mbele na zaidi ya umeme wa kutosha kuuza nje.
Sarakasi zikaanza ghafla, kwanza tukaambiwa gharama za umeme hazitashuka na huenda zikaongezeka tofauti kabisa na kile tulichoaminishwa hapo mwanzo kuwa, mbali na uhakika wa kupata umeme basi tutapata unafuu mkubwa wa kuilipia hiyo nishati.
Soma Pia: Rais Samia: Serikali itanunua Umeme nje maalum kwa Mikoa ya Kaskazini
Hatujakaa sawa, umeme ukaendelea kukatika ovyo ovyo mara kwa mara, sababu ikaelezwa ni kuwa ni kutokana na kuchakaa kwa miundo mbinu ya usambaji wa umeme ambayo inahitaji ukarabati mkubwa na endelevu hivyo tuwe wavumilivu maana baada ya muda miundo mbinu itatengemaa na hicho kilio kitasahaulika.
Sasa ghafla leo tumesikia mpango mpya wa serikali kutia saini mkataba mpya wa kununua umeme kutoka nje ya nchi (Ethiopia) ili kuweza kutatua changamoto za kukatika katika ovyo umeme hapa nchini hususani kwa mikoa ya Kaskazini. Hivyo changamoto ya kukatika katika ovyo umeme itakwisha kwa kununua umeme kutoka Ethiopia na sio tena kukarabati miundo mbinu chakavu ya usambazaji wa umeme hapa nchini!
Kuna namna hatuko serious!