Salam wanajamii wenzangu. Naamini humu hakuna wachoyo wa msaada wa mawazo. Ni kwa matarajio haya naomba kuuliza mimi nafanya kazi sekta binafsi kama mwajiriwa mwisho wa mwezi naweza ku save laki mbili na nusu
Ninauliza hivi kwa kiasi hiki ninawezaje kukitumia ili angalau miaka michache ijayo niweze kuwa na kabanda kangu na kisha angalau kamkoko kamoja kupunguza adha ya usafiri hapa mjini
Nawashukuru sana
hicho kiasi mkubwa ni baada ya kutoa gharama zingine kama kuendesha familia, usafiri na mengineyo. Yaani huwa nabakiwa na mshiko huo baada ya kugaharamia vitu vyote muhimu vya mwezi
Kwanza nakupa hongera kwa kujenga utamaduni wa kujisevia, ili ufanikiwe kusevu vitu 3 muhimu lazima uwe navyo: NIA, Utekelezaji na Kuamini. Kisha:
1. Uwe na malengo (goals) - andika "blueprint" in details yale yote unayokusudia kufanikisha katika muda ulioupanga. Ila uwe realistic mfano baada ya miaka 5 uweze kumiliki nyumba ya millioni 15 mpaka 20 na sio ndoto ya hekalu la billioni 3.
2. Andaa strategies na routine na ukomae nayo, usitetereke: Lengo katika hili ni kubana matumizi na kuifanya saving yako iongezeke zaidi, unapoanza kujisevia jambo la kwanza muhimu sana kujifunza ni ujanja wa kujua nini tofauti baina ya "thamani"(Assets) na "hasara" ( liabilities) thamani = kitu ambacho kina uhakika wa kuongeza kipato na hasara = kile ambacho kinahitaji fedha kujiendesha na hakileti tija, mfano mtu kakuuzia dhahabu bei bwerere hio ni thamani, gari ya millioni 7 inauzwa kwa millioni 3 hio ni thamani, ila unatakiwa uwe mjanja na makini sana katika hili. vitu kama TV, Hi-Fi system, Fenicha, gari ni hasara kwa sababu gari linahitaji mafuta, Tv, fenicha hata ukitaka kuuza ni taabu na mara nyingi hautopata faida, ni bahati hata ku break-even.
3. Live frugaly - Matajiri wa kujitengeneza wengi wamefika huko kwa sababu waliishi kwa kujibana - sisemi kama unataka utajiri ila the same rules apply for Savers, Kama ulikuwa unakula chips kuku kila usiku, jitahidi iwe alau usiku mmoja na badala yake uanze kujipikia, andaa bajeti yako ya kula kila wiki na uangalie wapi unaweza kubana zaidi, mfano kama unanunua viungo gengeni, jaribu kwenda pale sokoni usiku mmoja k/koo na ujinunulie kwa jumla. Kama mtu wa ulabu punguza mahudhurio Pub, jinunulie jumla bia zako kwa wiki na utulie nyumbani usiku.
Ukizingatia haya ambayo ni basics bila shaka utafanikisha malengo, wengi tulianza hivi hivi mpaka kufikia kumiliki vibanda nk.