Kaka hauko pake yako,ila kwa uzoefu tunatofautiana,mwenzio hisia za mapenzi zilikufa pale mchumba wangu aliponisaliti na nikajidai kupoza machungu kwa kuwa mlupo bahati nzuri sikuyakanyaga,mwisho nikajiuliza kama sitapenda tena ni nani atakayekuwa mama wa watoto wangu..??Nikatafuta mtaalamu wa ushauri na sasa niko katika hatua nzuri tu ya kutengeneza uchumba na mungu akijaalia ndoa itafuata kwa mchumba ambaye nimekutana naye hapahapa JF.Tafuta washauri watakusaidia,kwa kuanzia nenda pale Muhimbili kama uko Dar,kuna kitengo cha Wendawazimu,ulizia kuna wataalamu wazuri sana na nina imani wanaweza kukusaidia katika tatizo lako..