Nimeshawahi kusoma makala kuhusu asili ya maneno "baba" na "mama". Mwandishi alikuwa anahoji "m" ndio herufi ya alfabeti ambayo ni rahisi kushinda zote kuitamka, hata haja ya kufungua kinywa hakuna. Ndio maana aghalabu ni mojawapo wa herufi za kwanza mtoto atamkazo. "a" nayo ni mojawapo wa herufi hizo kwa sababu ya urahisi wa kuitamka.
Sasa, sababu ya mama kuitwa "mama" ni kuwa mtoto huwa anakuwa anatamka sauti mbalimbali randomly ambazo kati ya hizo "ma" ni sauti irudiayo mara nyingi. Kwa hiyo, atumikaye muda mwingi zaidi kwa ajili ya malezi ya mtoto (ambao aghalabu ni mama yake) aliona mtoto often anaitamka sauti ya "ma" repetitively amwonapo, alifikiri ndio jinsi mtoto aliamua kumwita na mama naye alianza kujiita "mama". Hivyo, "mama" likakubaliwa kuwa jinsi mama anavyoitwa.
Halikadhalika, mwandishi alifanya conclusion kwamba neno "baba" likafika kuwa jina la mtu wa mbili atumikaye muda mwingi na mtoto (ambao huwa ni baba yake) kwani sauti ya "b" utamkwaji wake nao ni rahisi sana (ukilinganishwa na sauti zingine za alfabeti) lakini si rahisi kama sauti ya "m" na "a".
Sijui kama etymologists wengi wanakubali na hilio, lakini inaonekana kuwa nadharia yenye mantiki.