Hivi mafaniko ya Club za mpira wa bongo ni kuwa na "Day" tu?

Abuu Kauthar

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2011
Posts
4,296
Reaction score
6,492
Wadau habari,

Ukikaa chini ukatafakari na uhalisia wa mambo yanavyoenda unaona kichefuchefu kabisa, na kama una mimba changa unatapika kabisa.
Yaani timu kubwa bongo simba ya yanga ni uharo, haiwezekani timu zinazeeka halafu hazina cha maana cha kujivunia zaidi Simba kuwa na Simba day, wakati yanga wao wanalilia kupewa vifaa na wadhamini.
Mbona mambo haya sioni kule uingereza Man United au Arsenal wakipewa vifaa vya michezo na wadhamini wao?
Jana PSG walikuwa wanauza jezi za Neymar kwa karibu shilingi laki tatu za kitanzania. Na jana tu wameuza jezi karibia laki mbili, sasa wameshindwaje simba kuwa na utaratibu kama huu angalau kuuza jezi shiling laki moja za john Bocco?
Wadau hakuna namna ya kuvi-ban hivi vilabu kweli tupumzike?
 
mkuu ucwaambie ukweli
wanalilia jezi duh!!!!! ndo Mara ya 1 nasikia
kwa mtani msimu huu patachimbika
 
Haina shaka kuwa unahitaji kutafakari upya mawazo yako unapolinganisha Simba na Man au Asenal au PSG . Mpira ni ule ule kanununi ni tofauti kule ni pro na hapa ni semi pro lazima kuwe na tofauti . Huhitaji miwani kuliona hilo jua kuwa wachezaji wetu ni Amature and some profeshono ambao hata kodi sijui kama umewahi kusoma mahali wanalipa
Hii ni dunia ya tanganyika na zanzibar

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mie nishawahi kushauri hapa,waanzishe fan club yao,wauze saa za ukutani,foronya,skafu,soksi na hata kuwa na app yao watu watabiri mechi,hivi vitu ni simple vya kuongezea kipato chao,wengi wakishastaafu wanakuwa na maisha unpredictable,wakati vitu vingine ni simple kuvifanya.
 
Sinaga ushabiki kwa kweli na timu hizi kwan hazina khabar mpya wachezaji ni walewale wanafanya kubadilishana tu msimu huu Simba ujao yanga bas ndo wameishia apo mwishowe utaskia mchezaj yupo lipuli au ndanda na hatimae wanapotea tu kitaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nakushauri upumzike mwenyewe sio lazima kua shabiki wa team za kibongo. shabikia hao wazungu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usitoe shutuma za hovyo hovyo zisizo na mpangilio. Kwanza mashabiki wa Kitanzania sio kama wa Ulaya in terms of Kipato. Jezi zetu halisi zinavaliwa na wachache. Pili jina Lindi la Wafanyabiashara wasio waaminifu wanaodurufu jezi Bandia na kuuza. Ulaya hakuna jezi Bandia.

Simba wameanza kuuza jezi mpya. Zinapatikana Klabuni Msimbazi Tsh 30,000/= . Wamesema ni um kwa ajili ya Simba day. Wenye jezi mpya watapata favour zaidi. Lakini naomba nikuulize ukadhani Watanzania wangapi wanaweza kumudu kununua jezi Tsh 30,000/=? Siku si nyingi zile Bandia za kuuzwa jwa mafungu Tsh 10,000/= zitatoka. Klabu haitafaidika.

La pili unazungumzia kwa kuinanga Simba Day. Kwanza huu ni ufupi wa mawazo. Simba Day ni tamasha la kila mwaka kutambulisha jezi mpya na wachezaji wapya. Ni income generating activity. Kwa Simba Day peke yake klabu inaweza kuingiza Milioni 200 . Halafu unaanza kutoa malalamiko yasiyo na kichwa wala miguu.

Tatu mafanikio ni relative. Kuna timu Ulaya ni kubwa lakini relatively hazina mafanikio yoyote. Niambie timu kama Spurs ina kipi cha kujivunia ndani ya England na Ulaya kwa ujumla? Arsenal mbali ya kutwaa FA CUP ambalo ni local cup ndani ya UK ina mafanikio gani nje ya Uingereza? Man City ukiachana na ubingwa wa Uingereza ambao status ni kama ubingwa wa Vodacom tuuu one mafanikio gani nje ya Uingereza?

So unaposema mafanikio unatakiwa utambue hilo ni relative.
 
Kwa ujinga wako huu hizi timu za bongo zitaishia hapo hapo simba day hutokaa uone inachukua hata kombe la shirikisho tu, na michuano ya kimataifa kwa timu ya taifa nayo itabaki kichwa cha mwendawazimu maana akili uliyonayo ndio walioyonayo viongozi wako wa mpira pia.
 
Nafikiri hapa ni jukwaa la wenye hekima. Mtu mwerevu daima hatoi matusi. Pinga hoja kwa hoja. Umeelezwa changamoto kadha wa kadha wewe unafikiri mpira ni kazi rahisi. Azam imeanzishwa juzi na mkadhani ni model bora, ina kila kitu kuanzia uwanja mpaka Fedha, ina mafanikio gani unayodhani yanakuja kirahisi? Unatakiwa utambue mbali ya fedha hata Ligi yenyewe ya Tanzania yawezekana sio bora enough kutoa bingwa anayeweza kupambana vyema huko nje.
 
we unaleta mada zilizojaaa matope halafu unategemea majibu ya cement. dawa ya moto ni moto jaribu utasema ndio.

Sent using Jamii Forums mobile app
Usiumize kichwa chako. Huyu jamaa ni mmoja wa watu wanaoishia kuwasoma kina Shaffih Dauda na Edo Kumwembe halafu anakimbilia kuanzisha thread. Mpira wetu una changamoto nyingi sana kuanzia uendeshaji, viwanja, wachezaji, waamuzi, ratiba na mengineyo. Tunaweza kuwa na mabingwa na wenye fedha nyingi kama usemavyo lakini tusiwe na timu bora nje ya Tanzania. Anatakiwa ajue kwanza changamoto zetu ni zipi ndio ushauri namna bora ya kuzishughulikia. Ligi mbovu, timu zinazoshiriki ni dhaifu, wachezaji hawana vipaji, udhamini ni mdogo kwa vilabu vidogo halafu unatarajia bingwa awe bora?
Tuliona msimu uliopita wachezaji wa timu kama Stand United, Majimaji, Toto na zingine wakilalamika kutolipwa fedha za mishahara na posho zao. Mbeya City mpaka wachezaji wale Waganda walifika Ofisi za gazeti la Mwananchi kuomba msaada, halafu utarajie wawe competitive na kutoa ushindani bora?

Ni rahisi sana kutoa lawama kama shabiki hasa wa timu pinzani dhidi ya wale wenzie wenye kufanya walau hatua moja katika safari ya maili elfu moja. Daima hutoa hoja dhaifu kuwakwaza.
 
Msitafune maneno..liserikali LA CCM ndio chanzo cha yote..Manji na Mo walitaka kuchukua timu ziendeshwe kisasa wakawakatalia.Huwezi kushindana na timu kama TP Mazembe .Mamelodi.Timu za Misri.Tunisia .Morocco kwa Msuva na vibajeti vidogo...Timu zote duniani zinamilikiwa na matajiri wakubwa..bongo bahati mbaya
 
Ujinga c tusi, na hakuna mahala nimetukana...miaka 60 sasa tangu tupate uhuru eti tunajikongoja. Tatzo lenu hampendi kuambiwa ukweli, mkiambwa ukwel mnatoa visingizio lukuki kama hvyo hapo ulivyotaja ili mwisho wa siku mnataka tuwaache muendelee kunufaisha matumbo yenu. Sawa endeleeni.
 
Hukawiagi kusema wewe ni mshabiki wa majimaji

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…