Hivi Mafuta huwa yanapandaje bei?

Hivi Mafuta huwa yanapandaje bei?

Emmanuel180

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2019
Posts
342
Reaction score
626
Binafsi hua nashangaa sana sipingani na kupanda kwa bei ya mafuta lakini hua nashangaa mchakato unavokua

Mara nyingi EWURA ndio hutangaza bei mpya lakini sijawahi kuona wakitangaza bei mchana mpya wanatoaga taarifa USIKU wa manane asubuhi unaamka unaambiwa tu mafuta yamepanda unaenda kununua bia unaambwa 2000 badala ya 1500 kwasababu ni asubuhi una hang over unabaki ume duwaa huna cha kuchangia maana yamepanda toka jana usiku.

Lakini sasa hua inakuaje serikal inatangaza kupanda kwa bei usiku asubuh zishapanda kila mahali je ni kweli hao wafa ya biashara wanakua na hio stock moja ya mafuta iliopanda bei dakika chache hivooo wasiwasi wangu hiii serikal ya sahv inaumiza wananchi wa kawaida na ina wa favour wenye nacho mfanya kwenye biashara shilingi 200 kwenye kila litre ya mafuta ni pesa nyingi sana.

Kinachonishangaza EWURA wanatangaza sasa hivi after 5 mins iring kigoma njombe DSM kote zishapanda why
Inamaanisha wahapata hio stock mpya na wao.
 
Sio yanapanda,yanapandishwa bei na wazalishaji kulingana na demand ya soko na uhaba uliopo sokoni
Kwaio hawa suppliers wetu hua wanaenda sokoni kila siku? Ninachooongelea hapa wewe leo unaweza kua na biashara ya duka una sukari mifuko 500 kilo 2500 inatokea unaongeza bei ya sukari 3000 kwa sababu sehem zingine zimepanda ilihali wewe hukununuliaa bei hio
 
Kinachonishangaza ni huu utaratibu wa kupandisha bei kila mwezi. Sijui mpumbavu aliyeleta hili wazo alitumia kiungo gani kufikiria
 
Maendeleo hayana Chama. Wacha waisome nambaaaaaa eeeeeeeh wajinga waleeeee. Maliziaaaaaa naniliiii ni ileeeeeileeeeeeee.

#teamWalambaAsali
 
Kwaio hawa suppliers wetu hua wanaenda sokoni kila siku? Ninachooongelea hapa wewe leo unaweza kua na biashara ya duka una sukari mifuko 500 kilo 2500 inatokea unaongeza bei ya sukari 3000 kwa sababu sehem zingine zimepanda ilihali wewe hukununuliaa bei hio
Una hoja Ila sasa mkuu tukichukulia kwa muktadha huu itabidi mwenye amana hiyo aiuze akiogopa dhulma tofauti na hivyo kama hana utu atataka kujitajirisha kupitia uchochoro huo.

Pesa na imani ni vitu viwili tofauti matajiri wanawanyonya sana maskini hasa kwenye serikali zinazoongozwa na viongozi kama hawa wa kwetu.
 
Kwaio hawa suppliers wetu hua wanaenda sokoni kila siku? Ninachooongelea hapa wewe leo unaweza kua na biashara ya duka una sukari mifuko 500 kilo 2500 inatokea unaongeza bei ya sukari 3000 kwa sababu sehem zingine zimepanda ilihali wewe hukununuliaa bei hio
Wanaagiza yanapozalishwa,kwanza gharama za shipment,pili uhitaji wa soko na kulingana na current crisis btn ukraine na russia,kwani inaaminika kuwa russia ni mzalishaji mkuu wa mafuta,tatu ajeti ya akiba kwa mataifa yenye ukinzani na russia hasa ukiangalia sanction ya mataifa ya ulaya kwa urusi.
 
Back
Top Bottom